Wassira: Mnataka serikali za majimbo mnafahamu zilivyo na gharama au mnaigiza tu

Wassira: Mnataka serikali za majimbo mnafahamu zilivyo na gharama au mnaigiza tu

Huyu mzee Wasira akili ishazeeka mwambieni apumzike.
Hakuzeeka yeye tuu, bali na CCM imekwisha zeeka mno.
Kila kitu husimama kwa misingi yake,
Msingi huwekwa mara moja tuu .Msingi wa SISIEMU ni dhaifu mno wenye dira za kumtowa mkoloni,hofu yao siku zoto ni mkoloni kurudi.
WAFUATILIENI kwenye hotuba zao?
Kila kitu CCM wanakipa taswira ya Mkoloni.
Pili wanasingizia Umoja wa kitaifa wakati wao ndio wanauvunja.
CCM kwishneh Haina Sera Ya TAIFA wala DIRA
 
Kuna majimbo 13 Marekani yenye udogo wa chini ya km² 100,000. Tunaweza kuwa na majimbo 10 tu, sio 50 kama Marekani.
 
Huyu mzee ameanza anataka kutuharibia nchi kisa tumbo na tamaa zake,atupe hizo gharama halisi za majimbo ukilinganisha na gharama za kuendesha nchi kwa bajeti ambayo hata 50% haijawahi fikiwa.

Wazee kama hawa hawafai ni wanazi na waliojaa uhafidhina.
Ungemjibu hoja yake na si kumshambulia. Kwani Babu yako hajazeeka au babaako hatazeeka? PUMBAVU!
 
Texas ya wapi iko sawa na TZ huyu mzee!!? Kwanza serikali za mikoa na wilaya za sasa mbona ni serikali kamili. Zina kila kitu na idara za kuwa serikali kamilifu. Gharama za kuziendesha zikoje? Waseme hawataki wakazi wa eneo husika wajiamulie masuala yao ya maendeleo. Wanachotaka ni fedha zote ziingie magogoni na waanze kuzitoa kama zawadi na takrima.
 
Na hizo Halmashauri ndogo ndogo za wilaya zinaunganishwa ndizo zinakuwa mabunge ya majimbo.
Serikali za majimbo ni cheap zaidi kuliko muundo wa sasa.

Chadema inachosema ni kwamba hizi kanda za hivi Sasa ndiyo ziwe majimbo (mfano kanda ya ziwa yenye mikoa zaidi ya 5 ) iwe Jimbo moja.

Chukua hiyo mikoa 5 Ina wakuu wa mikoa 5, wakuu wa wilaya zaidi ya 40, maRAS 5 , maDAS 40, maDED 40, maDEO 40, maREO 5, maRPC 5, maOCD 40, wabunge 60, n.k

Serikali ya Jimbo ni cheap mno kuliko ilivyo hivi Sasa. Huyu mzee Wasira akili ishazeeka mwambieni apumzike.
 
Mbona Kenya hakuna mgawanyiko?
Majimbo yatasababisha mgawanyiko na hata kutaka kujitenga. Tumeona Ethiopia vita kali ya kutaka kujitenga jimbo la tigray kaskazini ya nchi hiyo. Pia Nigeria hakuna usalama wala utawala bora kutokana na majimbo. Huku mashariki majimbo yaliyowahi kupigana vita ili kujitenga na kuunda nchi ya biafra kwenye miaka ya 60 leo yameanza tena kupigana kutaka kujitenga.
 
Sasa garama zikiwa kubwa situmeambiwa tutakatwa tozo kwa manufaa ya nchi yetu?

Hata wafanye kilajimbo liwe na Rais wafanyetu hivyo
 
Majimbo yatasababisha mgawanyiko na hata kutaka kujitenga. Tumeona Ethiopia vita kali ya kutaka kujitenga jimbo la tigray kaskazini ya nchi hiyo. Pia Nigeria hakuna usalama wala utawala bora kutokana na majimbo. Huku mashariki majimbo yaliyowahi kupigana vita ili kujitenga na kuunda nchi ya biafra kwenye miaka ya 60 leo yameanza tena kupigana kutaka kujitenga.
Usijiite great tinker km wewe ni shallow thinker. Hizo sehemu zote ulizotaja Zina historia ya ukabila tangu enzi na hawajawahi kupata muafaka wa kudumu na ni maeneo yanayokaliwa na aina moja ya kabila linalohitaji kujitawala. Kwa Tanzania tungefananisha na kabila la Wasukuma baada ya uhuru walitaka Kisuma ndio iwe lugha ya Taifa kwa sababu ya wingi wao. Lakini Mwlm Nyerere kawaminya sehemu nyeti wakatulia ndiyo kikatangazwa Kiswahili lugha ya Taifa ili kuondoa ukabila. Ndiyo maana Mwlm Nyerere alikemea sn watu kuulizana kabila.

Kwa mazingira ya sasa Tanzania haiwezi kuwa na ukabila. Mfano kanda ya Ziwa ina makabila karibu 100 sasa hapo kwa utaratibu wa utawala wa Majimbo utaleta vipi ukabila. Watu wasifananishe nchi zenye makabila machache makuu na Tanzania isiyo na kabila kuu kuliko lingine.

Someni historia msidandie vitu. Archives zipo kwa ajili ya watu kupata maarifa. Mnang'ang'ana na Biology wakati hata nguvu za kiume hamna.
 
Huo msumari wa moto kweli, tunaposema wazee ni hazina tuelewane tu palipo na wazee haliharibiki jambo.

CHADEMA ni weupe sana kichwani, unapouzungumzia serikali unazungumzia mamlaka kamili yenye kila kitu ndani yake. Sasa wanajiokotezea vitu impractical mitandaoni wanataka ku practice kwetu

Majimbo vs uongozi wa mkoa na wilaya pamoja na madiwani [emoji848]
 
Back
Top Bottom