Wastaafu wa Dar es Salaam walalamika fedha nyingi zinawachanganya

Wastaafu wa Dar es Salaam walalamika fedha nyingi zinawachanganya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FcDItf-XgAAOf-n.jpg

Wastaafu zaidi ya 5,000 Mkoani Dar es Salaam wamesema wanapata shida katika uzee wao kwani hawana elimu ya matumizi ya fedha na uwekezaji pindi wanapofikia hatua ya kustaafu na kupewa pesa nyingi ambazo wengi huwa zinachanganya.

Hata hivyo katika kikao hicho ambacho Serikali kupitia Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imechukua jukumu la kuwakusanya wastaafu na kuwapa elimu ya fedha ili waweze kujinusuru katika umaskini ambao umewakuta walio wengi.

FcDJJLDXoAEeUBi.jpg

Source: EA Radio
 
Kila mstaafu anajua cha kufanyia hela yake, hata akiamua kuhonga hayawahusu
 
Kila mstaafu anajua cha kufanyia hela yake, hata akiamua kuhonga hayawahusu
Hela ya pensheni ni ya kijinga sana mimi ni shuhuda ninayeishi.

Wakipata hela nyingi wakizitumia vizuri tu hawa wazee wetu hawaishi zaidi ya miaka sita ila wakizitumia vibaya huwa wanaishi muda mrefu sana. Ni kama kakanuni hivi kwa niliowashuhudia na ni wengi
 
Duuh!! Kwamba unataka kusema nn hasa?
 
Hizi ndio Bange..., (Bangi), wewe ushastaafu ndio maana una pension tunakupa kidogo kidogo ili utumie na usiwe mzigo kwa jamii..., uzuzu ni kutoka kwenye shughuli na badala ya kulia kivulini kukimbia na kuhangaika sijui kuwekeza hapa na pale...

Hapo naona ni hio Benki ya Biashara inataka kuwatumia kama fursa kwa kuwapa vipackage vya ajabu ajabu na mwisho wa siku kuwakata kwenye monthly pensions zao hence kuwa mzigo tena wa jamii...

Tena hao wazee washukuru angalau wana-pension this crop wa hawa jobless wa sasa uzeeni hawajui wapi watapata hape senti za kununulia panadol
 
Back
Top Bottom