DOKEZO Wastaafu wa TAZARA tunasotea stahiki zetu huu Mwaka wa 20, Rais Samia tusaidie

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mama kumbe anatoa milioni 10 kuununua kila goli la simba na Yanga wakati Kuna watu wanadai fedha zao?

Huyu rais vipi hana vipaumbele??
 
Pesa zipo za magoli tu na kuwa safirisha mashabiki kushangilia team
Nyie wazee wa Tazara mtulie tu

Ova
 
Tazara Ina changamoto kubwa sana,ni sawa na mtoto aliekosa walezi...hadi kufikia Leo April 3 mishahara ya march haijalipwa na hakuna maelezo yakueleweka.
 
Na hili ndilo tatizo kuu..
Binafsi mzee wangu ni muhanga ktk hilo na nadhani yupo pa1 na mzee wako ktk kufuatilia suala hili.
Nilimwambia wakitaka kufanikiwa ktk hili waache kujinasibisha na ccm, badala yake wawatumie upinzani wenye sauti kuwapgia kelele.
Laah..
Nimeonekana mjinga na mtoto mdogo nisie mzalendo.
 
Kuna mzee wangu mmoja pia yumo kwenye hii issue , hawa wazee wanataabika sana . Mh. Rais tunaomba uangalie hawa wazee wanataabika sana.
 
Push back ya kupata katiba mpya,issue hii ingeenda kwenye mahakama huru na yenye kujitegemea na haki ingetolewa,waziri mhusika angewekewa garnish ya kimahakama na kuwajibishwa yeye binafsi kwa uchelewesho kwa sasa wazee wangu wa TAZARA mpo kaput moja na wazee wa EAC ,mtakufa mmoja baada ya mwingine
 
Mkiambiwa muandamane ili katiba irekebishwe tupate viongozi wenye hekima mnajifungia ndani.
 
Nakubaliana na wewe
 
Huo mchezo mchafu ,wa kunyima wastaafu haki ya msingi upo siku nyingi sana,kuna wale pia wazee wa kiwanda cha viatu(Bora) wamedai mpaka basi na hakuna aliyesikiliza kilio chao na kwa Sasa wengi wao ni marehemu.
Wakome mpk waanze kuandamana
 
Kwani ni shilingi ngapi kwa ujumla wake wanadai wazee hawa? Je, bilioni 10, 20 au 60?

Hata iwe shilingi ngapi, hivi hii serikali ya CCM inashindwa kweli kuondoa kelele za wazee hawa kiasi cha kuleta laana na balaa kwa taifa hili kwa kushindwa kulipa bilioni 20 au 60 tu katika hazina ya taifa tajiri kama hili la Tanganyika?

Hivi kweli wana CCM nyie hamuoni aibu wala haya kudaiwa na wazee hawa wakati waziri mmoja tu wa CCM anaweza kununua nyumba mbili au tatu Dubai na Johannesburg - South Africa kwa bilioni 20?

CCM hamuoni aibu? Hawa vigogo wa CCM na serikali yenu wanatoa wapi pesa nyingi kiasi hiki ndani ya muda mfupi wakiwa viongozi wa umma kama sio kuwaibia Watanganyika wakiwemo hawa wazee wastaafu wa TAZARA, wa umma na taasisi zingine za umma?

Jamani epukeni hasira ya Mungu. Tendeni haki. Acheni dhuluma. Vinginevyo, tambueni kuwa machozi na vilio vya wazee hawa na Watanganyika kwa wingi wao kimeshamfikia Mungu huko juu mbinguni anakoketi na yuko tayari kushuka na kuachilia ghadhabu yake dhidi ya viongozi wa serikali hii na taifa letu kwa ujumla..

Tafadhali CCM, watu tumeshaomba sana Mungu ili aachilie rehema zake. Lakini mbona hamsikii wala kutenda yawapasayo kutenda?

Tafadhali, hebu nyie CCM liepusheni taifa hili na balaa hii toka ktk ghadhabu ya Mungu. Fanyeni yanayowapasa kutenda sasa. Mna muda mchache sana uliosalia..!!
 
Nyinyi ndiyo wapiga kura nambari moja wa CCM, hongereni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…