Wastani wa gharama za kuhamisha Mtumishi mmoja wa serikali ni Mil 25

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Serikali inawezekana inatumia pesa nyingi sana kuhamisha viongozi na watumishi waandamizi wa serikali, Fedha hizo zingeweza kuelekezwa mahala pengine ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii.

Wastani kuhamisha Kiongozi/ mtumishi mmoja ni kuanzia mil 25 Hadi 40, lakini tofauti na nchi nyingine duniani Tanzania imeweka record ya matumizi makubwa zaidi ya kuhamisha watumishi kuliko nchi yeyote dunia hii.

Ukiachilia Fedha zinazotumika Kusafirisha viongozi nje ya nchi, matumizi ya kuhamisha watumishi imekuwa ni namba mbili, serikali Haina hasara, lengo la kuhamisha watumishi limekuwa likichagizwa zaidi na Siasa kuliko uhitaji wa kuhamisha viongozi hao.

Sasa serikali ijitathmini
 
Mtumishi sio kama diwani au mbunge kwamba ana wapiga kura wake hapo hawezi kuhama, anatakiwa kuhama ili kuongeza ufanisi na kupunguza mazoea. Standard asizidi miaka mitano
 
hapo dawa ni kubadilisha au kufuta sheria iliyoweka malipo hayo labda hio milion 25 ni kama unahamia nje ya nchi lakini kama ni mkoani lori mbili za jeshi zinatosha kabisa kuhamisha furniture na mabegi na watoto hayo mengine ni ufisadi tu uliohalalishwa kwa kutungiwa sheria.!
 
Watu wanashindw kuelewa.

Kumtoa mtu eneo moja akiwa na familia ni gharama sana.

1- Amejenga inabidi aache nyumba yake akapange
2- Ana biashara zake, aache akaanze moja sehemu nyingine
3- Watoto shule, aache ada akalipe nyingine sehemu atakayohamia.
4- Usumbufu
5-Gharama za kusafirisha vitu (vingine vitaharibika au kupotea)
6- kama ana Magari matatu yote yawekwe mafuta, service na madereva kulipwa posho yaende huko anapohamia.
7-Mke/Mme kama anafanya kazi hapo inabidi amuache aende mwenyewe.

Na mengine mengi.

Hayo yote yanatakiw yapewe Compensation.
 
Pamoja na kuhamishwa kila wakati lakini bado RUSHWA,UFISADI,UONEVU,UTEKAJI,UTENDAJI MBOVU,MAZOEA YA KIJINGA MAKAZINI,UKOSEFU WA MAJI,MIUNDO MBINU MIBOVU,UTATUZI HAFIFU WA KERO ZA WANANCHI ni Biashara as Usual!

Tulitegemea tengua tengua na hamisha hamisha ya watumishi mambo yabadirike but Business as Usually!

KAOLE SANAA GROUP
 
Serikali inawezekana inatumia pesa nyingi sana kuhamisha viongozi na watumishi waandamizi wa serikali, Fedha hizo zingeweza kuelekezwa mahala pengine ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii.
Wastani kuhamisha Kiongozi/mtumishi mmoja ni kuanzia mil 25 Hadi 40, lakini tofauti na nchi nyingine duniani Tanzania imeweka record ya matumizi makubwa zaidi ya kuhamisha watumishi kuliko nchi yeyote dunia hii.

Ukiachilia Fedha zinazotumika Kusafirisha viongozi nje ya nchi, matumizi ya kuhamisha watumishi imekuwa ni namba mbili, serikali Haina hasara, lengo la kuhamisha watumishi limekuwa likichagizwa zaidi na Siasa kuliko uhitaji wa kuhamisha viongozi hao.

Sasa serikali ijitathmini
So mie mama akiniamisha tokaka chamwino rudi dar napata hii, ngoja nianze mchakato ,haya ndo maisha sasa , chamwino to dar then dar to kigoma ,kigoma to shinyanga , tiyari nimevuta used v8
 
Unaijua serikali ww...hizo pesa unaweza usipate mpk unastaafu au kufa kabisa
 
Serikali inawezekana inatumia pesa nyingi sana kuhamisha viongozi na watumishi waandamizi wa serikali, Fedha hizo zingeweza kuelekezwa mahala pengine ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii.
Wastani kuhamisha Kiongozi/mtumishi mmoja ni kuanzia mil 25 Hadi 40, lakini tofauti na nchi nyingine duniani Tanzania imeweka record ya matumizi makubwa zaidi ya kuhamisha watumishi kuliko nchi yeyote dunia hii.

Ukiachilia Fedha zinazotumika Kusafirisha viongozi nje ya nchi, matumizi ya kuhamisha watumishi imekuwa ni namba mbili, serikali Haina hasara, lengo la kuhamisha watumishi limekuwa likichagizwa zaidi na Siasa kuliko uhitaji wa kuhamisha viongozi hao.

Sasa serikali ijitathmini
ni jambo la kawaida kwenye utumishi wa umma lakini pia haliepukiki 🐒
 
Serikali inawezekana inatumia pesa nyingi sana kuhamisha viongozi na watumishi waandamizi wa serikali, Fedha hizo zingeweza kuelekezwa mahala pengine ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii.

Wastani kuhamisha Kiongozi/ mtumishi mmoja ni kuanzia mil 25 Hadi 40, lakini tofauti na nchi nyingine duniani Tanzania imeweka record ya matumizi makubwa zaidi ya kuhamisha watumishi kuliko nchi yeyote dunia hii.

Ukiachilia Fedha zinazotumika Kusafirisha viongozi nje ya nchi, matumizi ya kuhamisha watumishi imekuwa ni namba mbili, serikali Haina hasara, lengo la kuhamisha watumishi limekuwa likichagizwa zaidi na Siasa kuliko uhitaji wa kuhamisha viongozi hao.

Sasa serikali ijitathmini
Kwa faida yangu na wengine naomba utuwekee mchanganuo wa hizo garama ili roho iniume zaidi 🙌🙌
 
Back
Top Bottom