Wastara afunguka kuwachukia wanaume wenye rangi nyeupe

Wastara afunguka kuwachukia wanaume wenye rangi nyeupe

Siku ZOTE wanawake wanawapenda WANAUME Warefu na weupe... ukiona hivyo UJUWE KISHAUMIZWA na weupe... Anaona bora awe na weusi... Hatopata STRESS.... KUMBE keshasahau kwamba hata sisi wanaume TUNACHAGUWA PIA...
 
Hivi kuna watu wakikua ndo wanakuwa hawajitambui?!
 
Huyu wastara dishi limeshayumba ni wa kuombewa kabisaaaa... Mara aseme mgongo wake huwa unahama.... Mara tena kashawahi kumwona zirailu Mara mbili yaan huyu dada ni mwehu
 
Ubaya wake ukimdai risiti yeye anadai talaka...hata hajapona kishawaza kulala na mtu bila nguo kweli kuna watu ule mchezo kwao kipaji
 
Mi mwenyewe nawachukia mademu wenye rangi ya njano.
 
View attachment 715517
Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amedai anawachukia wanaume wenye rangi nyeupe kwasababu wanakuwa na matatizo mengi pindi anapokuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi ndio maana kwa sasa anawapenda weusi kama aliyokuwa nayo marehemu Sajuki.

Wastara amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu miongoni mwa maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mashabiki zake waliokuwa wanataka kufahamu ni mwanaume wa aina gani Wastara anamvutia kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi au kwa sasa endapo atatokea.

"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambae anajiamini ambae hata tukitembea mbele za watu hawezi kuona aibu, anaejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe mwanaume wa kweli yaani asiwe 'Punga' ila asiwe na rangi nyeupe maana nawachukia sana wenye rangi hiyo, nampenda mwenye rangi nyeusi", amesema Wastara.

Aidha, Wastara amesema kipindi cha awali alipokuwa anaanza kujihusisha katika masuala ya mapenzi alikuwa na vigezo vingi alivyokuwa anavitaka awe navyo mwanaume kama kifua kikubwa, Six Pack na vinginevyo.

"Kwa sasa sitaki vigezo kwasababu nimejifunza mengi kutoka kwa marehemu Sajuki maana mume wangu alikuwa na Six Packs za ukweli lakini alipokuwa anaumwa zote zikaondoka 'so' kutoka hapo nimejifunza kupenda jinsi mwanaume alivyo maana vingine vinakuja na kuondoka wakati wote", amesisitiza Wastara.

Kwa upande mwingine, Wastara amesema yupo tayari hata sasa kuolewa na mwanaume mwingine ambaye wataridhiana wenyewe kwa kuwa dini yake ya kiislamu inampa fursa ya kuolewa mpaka pale kifo chake kitakapomchukua endapo hatakuwa katika ndoa.


Muungwana
Anachagua utadhani ni mwanamke mxur,wakati hana uzuri wowote
 
Huyu dada jamani fyuzi moja imeachia huko kichwani. Kila siku ana jipya. Wakitoka wanaume weusi atahamia kwa wanawake sasa.
 
Siku ZOTE wanawake wanawapenda WANAUME Warefu na weupe... ukiona hivyo UJUWE KISHAUMIZWA na weupe... Anaona bora awe na weusi... Hatopata STRESS.... KUMBE keshasahau kwamba hata sisi wanaume TUNACHAGUWA PIA...
😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom