Wastara anunua gari mpya

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
CHEREKO!

Ikiwa umepita mwaka mmoja tangu mumewe Juma Kilowoko ' Sajuki ' afariki dunia , msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma ameongeza ndinga mpya na kuiacha ile ya zamani kwa muda.

Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma . Akizungumza na paparazi wetu, Wastara alisema gari hilo aina ya Toyota Cami alinunua kwa shilingi milioni kumi na tano na anamshukuru Mungu kwani fedha hizo zimetokana na muvi zake hivyo kwa sasa anamiliki magari mawili .

"Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunipigania kwani mafanikio haya siyo kwa nguvu zangu bali ni kwa neema yake tu, ukweli kazi ya filamu inalipa ndiyo maana naipenda kwani gari hili limetokana na filamu zangu nilizocheza, " alisema Wastara.
 
Toyota Cami...millioni 15......whattt?..

Nisaidie kushangaa, maana mmh!! Mbona mil 15 unapata gari lenye hadhi na zuri kuliko hata hicho ki camy, na wala sidhan kama kwel kanunua mil hizo, labda 7, huyu nae kashaanza misifa ya ajabu
 
Si lake na yy si ndo kanunua tumuache ndo pesa alizolipa hizo
 
Kwani hawa watu wakinunua kitu lazima dunia ijue? hawawezi kukaa kimnya watu wakaiona? ushamba mwengine jamani....
 
Bei ya gari inatokana na quality/Grade,Gari yenye km chache na grade nzuri hata kama collora AE100 bei yake itakuwa kubwa tu,msikariri sana GX100 ya 0km inauzwa 36,000usd zaidi ya 50m CIF ukija kwenye kodi majanga lazima uongeze nyingine 50m
 
Mil 15 si angenunua toyota Rush, hakuna Cami ya million 15, anyway labda ni ya mwaka huu na ina 0 km

Nisaidie kushangaa, maana mmh!! Mbona mil 15 unapata gari lenye hadhi na zuri kuliko hata hicho ki camy, na wala sidhan kama kwel kanunua mil hizo, labda 7, huyu nae kashaanza misifa ya ajabu
 
15 cam? bora angechukua verosa auze sura mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…