Wastara atoa sababu ya ndoa yake na kigogo wa CCM kuvunjika

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Msanii wa filamu bongo ambaye hivi karibuni amekuwa akipokea michango kutoka kwa watu mbali mbali kwa ajili ya matibabu, ameweka wazi moja ya sababu iliyofanya ndoa yake na kigogo wa CCM Sadifa Khamis kuvunjika baada ya muda mfupi.

Akizungumza na mwandishi wa eatv Wastara amesema mume wake huyo alionesha kutojali matatizo yake na badala yake kuweka pesa mbele, baada ya kudai risiti za matibabu aliyoenda kutibiwa India, kwa hela za michango ya watu mbali mbali, ili arudishiwe na bunge na ziingie mfukoni mwake.

Wastara amesema kitendo cha Sadifa kudai risiti hakikukifurahia, kwani pesa aliyokwenda nayo haikutoka mfukoni mwake, bali zilitoka kwa watu mbali mali wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Msanii Alikiba, rafiki yake Sadifa na wengineo.



Muungwana
 
Yaan sijui wanawake kwann tuna roho ndg kiasi hiki.

Hivi heshima kwetu imekuwa ni tabu kiasi hiki? Mume kaomba risit hivi hiyo ni ishu ya kukufanya uvunje ndoa? Eti akarudushiwe na bunge hivi huyu asingekuwa mumewe hata iyo heshima ya mke angepata?

Aache ujinga
 
Haaahaaaa.....ndoa ndoano
 
Shukrani kwa kuliona hili ni wachache sana kuliona kama wewe.
 
Wastara aache uongo mbona kipindi kile hakuongea kaja kuongea saiv baada ya shutuma za upigaji kwa kutumia ugonjwa mguu.

Sadifa alimpa pesa kiasi kikubwa za matibabu ndo maana akakubali ndoa ya haraka haraka.
Alikaa hospitali siku tano na baada ya hapo Alienda Oman mwezi mzima akipost products za MARC kwa wateja na kuwaambia anashusha mzigo wa nguvu.

Insta inaumbua sana
 
Usiache hii tabia
 
Niliziona zile post zake nikashangaa hio honeymoon mbona anakula peke yake,full mashauzi picha kila kona.
Alikaa hospitali siku tano na baada ya hapo Alienda Oman mwezi mzima akipost products za MARC kwa wateja na kuwa Amina anashusha mzigo wa nguvu.

Insta inaumbua sana
 
Ikiingia mfuko wa kulia si bado inakuwa kwenye suruali ile ile tu. Au...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…