Wastara: Nataka kuolewa na bilionea sasa hivi

Wastara: Nataka kuolewa na bilionea sasa hivi

dada kubwa we hutaki zilionea??
hela zinakuwa zingi zingi!!
ha haaa, mdogo wangu.....
kwani Mungu aliponiumba na akili na utashi kama hao wanaume alikuwa kichaa? si alijua na mimi naweza tafuta hizo zilionea zangu mwanyewe?
yaani kabisa nalala nasubiri mtu wa kunilitea hela zingi zingi kwa ujira wa k? kabisaaaaaaa!
kweli tumetofautiana aisee
 
Wastara Juma. IKIWA ni takribani mwaka mmoja tangu alipoondokewa na mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema sasa yupo tayari kuolewa lakini sharti la kwanza la muoaji lazima awe mtu mwenye fedha zake. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wastara alisema, amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati muafaka wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake.
“Inatosha sasa, nadhani muda wa kuwa na mwenzangu umefika. Napenda huyo mwanaume awe mwenye huruma, upendo na kutambua thamani ya mke lakini ni vizuri akiwa mwenye kujituma na awe na fedha nyingi.
“Natamani kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo sitateseka, nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina mambo mengi. Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au Prado (aina za magari) kulingana na hadhi yangu.


“Kiukweli nitafurahi sana nikimpata mwanaume wa aina hiyo, maana nitakuwa na uhakika wa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisaidia katika shughuli zangu za sanaa,” alisema Wastara.

Amenipata aje tu ani pm
 
Mhh mabig...ni maneno ya Wastara hayo?kwel mwaka mpya umeanza..!kumpata bilionare atakae kupenda,kujal kaz yako,kukuheshm,na kukuthamin ts kinda hard ktk ulimwengu huu!'Mungu akusimamie
 
ha haaa, mdogo wangu.....
kwani Mungu aliponiumba na akili na utashi kama hao wanaume alikuwa kichaa? si alijua na mimi naweza tafuta hizo zilionea zangu mwanyewe?
yaani kabisa nalala nasubiri mtu wa kunilitea hela zingi zingi kwa ujira wa k? kabisaaaaaaa!
kweli tumetofautiana aisee
Hii inaitwa busara mingi mingi!!!!!
 
Hii inaitwa busara mingi mingi!!!!!
ha haaa, rafiki lazima ku-acknowledge mapenzi mingi mingi ya Mungu kwetu......
ndo maana Mungu alitupa kila kitu sawa sawa kasoro biolojia zetu...... na hizo biolijia hazina la zaidi ya matumizi yake, bhaaasiiiiiiii. kila mtu anaweza fanya mwenzake anachoweza, ni kuamua tu
 
Wastara..mbona Sajuki akiwa hai hukuwahi kumwambia kuwa unataka ajitume awe bilionea?? by the way mimi ni bilionea ila navusha ngada!! uko tayari??? maana tatizo si ni ubilionea tu na haijalishi umekujaje?
 
Wastara..mbona Sajuki akiwa hai hukuwahi kumwambia kuwa unataka ajitume awe bilionea?? by the way mimi ni bilionea ila navusha ngada!! uko tayari??? maana tatizo si ni ubilionea tu na haijalishi umekujaje?

Mkuu usije kumfanya dada wa watu punda.
hizo ngada ufanywe mwenyewe lakin pesa ufaidi naye
 
Too bd for u mdada. Matatizo hayabishi hodi jamani, utampata bilionea after two month ni mgonjwa wa kugeuzwa kitandani hata raha ya hizo hela hataiona. Hela zinatafutwa tu jamani kubwa amtangulize Mungu katika kumtafute alie sahihi asije akajiona mwenye mabalaa tu huku duniani. Nampenda sn kwa misimamo yake mizuri,
 
Hey can't u make urself billionaire!? Mungu ni mmoja fanya kazi kwa bidii na muombe atakubariki achana na fikra potofu xa kufanikiwa kupitia mwanaume kwani wengi wa wanataka papuchi tu wakiipata wanasepa.
 
Wasanii wanahitaji washauri kabla ya kuongea kwenye media....
Neno moja linaweza kukushusha kabisaaaa...
 
Back
Top Bottom