Wastara: Sipo kwa ajili ya kujiuza

Wastara: Sipo kwa ajili ya kujiuza

Mwanamke ameshavaa gauni la harusi jeupe, la pinki, la kijani, la njano... Bado jeusi tu..
Ni aibu aibu aibu.... Kila siku ndoa za mkeka.
[emoji117] [emoji117] [emoji117] [emoji117] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] kaniki
 
wastara1.jpg


Staa wa Bongo Movie, Wastara Juma ambaye siku za karibuni aliomba talaka kutoka kwa mume wake amefunguka na kusema yeye sio mtu wa kujiuza, bali ni mtu ambaye anajijali na kujitunza.

Wastara alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS ambapo inasemekana kwa sasa kuna wanaume kibao ambao wanajitokeza kumtaka baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.

Msanii huyo amesema kuwa ni kweli wapo wanaume wengi wanaojitokeza kumtaka na wengine wakija na ahadi ya ndoa lakini bahati mbaya wanaume hao wanakuja wakati yeye haitaji kuwa na mtu kutokana na jinsi alivyoumizwa.

“Mimi si mali ya mtu na wala sipo kwa ajili ya kujiuza, lakini ukweli ni kwamba wapo wanaume wa aina nyingi ambao wanakuja na kunitaka wengine wanakuja wakitaka ndoa kabisa na wengine unakuta kweli wanania ya dhati kabisa lakini wanakuja wakati mimi sijisikii kuwa na mwanaume, maana kitu kwa kitendo alichonifanya Sadif hakijaniweka sehemu nzuri” alisema Wastara.

Source: eatv
Jana nimeona kusema akitaka kuolewa ataolewa muda wowote
 
Asigwa hiyo Avatar yako na maada zako mule mule kabisa
 
[emoji85] [emoji85] [emoji85] Utakuwa mgeni humu njini [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji43] [emoji87] [emoji15] [emoji15] [emoji57] hajitunzi wala nn ndoa salasini kidogo
Hahaha

Eb kuwa mkarimu kwa wageni
 
kama kweli na nafsini mwake ana nia njema ivo basi Mwenyezi-Mungu atampa bonge la mume zaidi ya marehemu sajuki kipenzi chake cha moyo.
 
Back
Top Bottom