Wastara: Wanasiasa wanatutumia kama Big G tu

Wastara: Wanasiasa wanatutumia kama Big G tu

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
Wastara.jpg


Staa wa filamu za Kibongo Wastara Juma, ameibuka na kusema kuwa wanasiasa wanawatumia wasanii wakiwa na shida zao lakini wakishapata uongozi huwasahau na kuwaona ni wasumbufu pale wanapohitaji msaada.

Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Wastara alisema kuwa kwa sasa wao watakuwa lulu kwa wanasiasa na kutumiwa ipasavyo lakini baada ya mchakato wa uchaguzi kuisha wataonwa hawafai, kitendo ambacho si kizuri kwani wanatakiwa kukumbukwa wakati wote.

"Yaani kuna wakati sipendi kabisa siasa na wala sipendi kufungamana na mtu kwa sababu nilichojifunza sisi wasanii tunatumiwa kama Big G tu kwa sasa kwa sababu wana shida, baada ya hapo tutaachwa solemba na hata tutakapohitaji kusaidiwa jambo lenye masilahi kwetu tutaonekana wasumbufu," alisema Wastara.


Chanzo: GPL
 
Hizi kauli mi huwa nazipinga sana
Muziki ni biashara kama biashara zingine bana,
Kama nina sherehe nitamlipa msanii atatumbuiza then tumemalizana, nikipata nyingine ntamuita tena
 
Kwa hiyo anataka kutuambia hawaezi kuamua jamabo nao ni kiyu au watu? ndio maana wanatafunwa tu?
 
Hizi kauli mi huwa nazipinga sana
Muziki ni biashara kama biashara zingine bana,
Kama nina sherehe nitamlipa msanii atatumbuiza then tumemalizana, nikipata nyingine ntamuita tena
kwani wasanii wanatakaje zaid iya hivyo? (Beli 9 anasema nilipe nisepe) hapo ndipo tulipo mm na ww
 
Back
Top Bottom