Salih
JF-Expert Member
- Jan 31, 2013
- 642
- 420
Leo nimepanda Basi toka Mkoa mmoja wapo wa Nyanda za Kusini naelekea Kanda ya Ziwa nikiwa na shauku kubwa kwakuwa tulipita njia ambayo nilikuwa nikiisikia sifa yake kuwa si rafiki hasa pale mkipata tatizo mnaweza kaa hata siku2 bila msaada, kufika eneo flani linaitwa Lupa wakapanda Wasukuma kama4 hivi, sasa wakaanza kupiga simu na wengine kupigiwa, mmoja alikuwa nyuma yangu, mwingine pembeni na mbele yangu, aisee hizo sauti naona walifikisha volume100%, nikaanza kujisachi labda kama nawezakuwa na ear-plug mfukoni nikakosa, nikatamani tufike sehemu network ipotee kabisa lakini wapi, inabidi kesho nikapime masikio, na safari nilio a mbaya na sipiti tena hiyo njia. Wasukuma mnaboa bhana.