Wasukuma tusaidie jamii zetu za wafugaji kuthamini elimu

Wasukuma tusaidie jamii zetu za wafugaji kuthamini elimu

Pilitoni

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
1,197
Reaction score
507
Moja ya mapungufu makubwa wanayoyafanya wasomi na wanasiasa wengi wanaotokea maeneo ya usukumani ni kwa kutotoa elimu stahiki kwa jamii zetu zilizo na utajiri wa kutisha kuthamini elimu.Hii ni dhambi kubwa na ni usaliti wa kutisha dhidi ya jamii zetu.Kila mmoja wetu sasa aamke kwa kila namna,tuhakikishe kuwa jamii zetu zinathamini elimu na ninaamini kuwa kupitia elimu maendeleo yatapatikana tu
 
Kwel mkuu juzi tu tumetoka kuzika kuna kijiji kinaitwa kwala ni kama Km 20 ukiacha morogoro road nilikutana na vitoto vya kisukuma vina chunga ndama na mbuzi vikiwa vimelowana na mvua iliyo kuwa ina nyesha nili viongelesha lakn havikuwa viki elewa vizur kiswahil nilisikitika sana pia sijajua kwa pale maeneo walikuwa wanaishi katika mazingira gan maana siku ona hat alama ya mji maeneo yale kweli lazima jamii zetu zibadilike Urithi wa mtoto ni elimu.
 
kweli kabisa ndugu, big up!
 
Upo sahihi kabisa mkubwa tena huku simiyu ni noma juzi tu jamii ya wafugaji wamewachalaza fimbo waalimu kisa kuna shirika liliwapa msaada wa viatu,wao wakadai ni vya freemason,wakalazwa chini na kuamliwa waombe msamahaa
 
hii ni kazi kwetu sote. jamii zote zinapaswa kuliona hilo na kulifanyia kazi. si kwa makabila ya kifugaji tu kama ulivyosema wewe
 
Ni kweli mkuu, sisi wasukuma wengi sana vijijini kwetu wanathamini mifugo kuliko elimu, na kama ikitolewa elimu ya kutosha, basi kupitia mifugo hiyo hiyo watoto wanaweza wakasomeshwa na kufika mbali kielim.
 
Back
Top Bottom