Nyinyi mnalipa kodi kila siku au haujui labda dubwe tu ndio hulipii kodi ila mchina analipia kodiMwisho mtasema mpaka wacheza kamari tuwe tunalipa kodi.
Hii imekuja baada ya yule jamaa kusema anasafisha kucha kwa laki 5 kwa kila kichwa kimoja na ana wateja kibao huko masakiDuh! Serikali imeamua kukaba mpaka penati daadeeki! Sasa kwa hao wachoraji watajisajili vipi wakati wale hufanya kazi zao mara chache zikijitokeza? Kwanza uchoraji ni mpana, wamelenga wachoraji wa aina ipi? Kuna fine artist, signwriter, painter, decorator, cartoonist, wachonga mihuri, wapaka rangi magari na majengo, ni wengi na wengine hawafanyi kazi hiyo kama kazi ya kudumu ya kila siku. Ni ngumu kusajili makundi kama hayo ambayo kazi zao hutokea mara chache chache very rare mtua hataona umuhimu wa kujisajili kwa kuwa anafanya kazi hiyo pale tu inapotokea. Labda hao wa salon maana wana mahali pa kupatikana. Kundi la wachoraji ni ngumu kulidhibiti kutokana na nature ya kazi zao
Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) katika jitihada za kutambua na kurasmisha kundi la vijana na mabinti wasusi na vinyozi limewataka kusajali rasmi na kutambuliwa
BASATA wanasema laZima ziwe kazi rasimi na walipe Kodi Kwa Serikali Kwa kutumia vipaji na sanaa zao za kusuka na kunyoa watu, laZima wachangie Pato la taifaView attachment 3480868
Hakika Watanzania wafundishwe kuwajibika kulipa kodiIsiwe lazima kujisajili, huyo anayetaka mikopo na fursa zingine za kazi yake hiyo aende tu BASATA akasajiliwe. Ukija kwa wasusi na vinyozi ni wengi tena wa madaraja tofauti, kuna wamama husikia nyumbani mtu mmoja, wawili, sio kila siku anapata vichwa vya kusuka. Hawa wenye masaluni makubwa, hair dressing, hair beuaut, hair cutting, barber shop maana hawa wana mpaka VIP salon na wanaingiza hela nyingi wateja nao ni wengi. Mchoraji anapata hela kiasi gani mpaka naye adhibitiwe kwa kusajiliwa na BASATA?