Wasusi na vinyozi lazima kusajiliwa BASATA

 
Hakika Watanzania wafundishwe kuwajibika kulipa kodi
hawakatai kulipa kodi, watalipa, serikali nayo inatakiwa iwaboreshee mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo namna ya kuboresha kazi zao na iwape mikopo isiyo na riba kuwezesha wengi kupata vifaa vya kufanyia kazi hizo
 
sawa, hakuna ubishi watachangia
 
Mi nataka kujua, walengwa hasa ni wasusi na vinyozi wa hadhi gani? Maana kuna saluni za VIP bei yake ipo juu sana tofauti na saluni za mitaani bei ya kunyoa ni buku tu, kusuka kuna misuko hadi ya jero, madraya hadi buku mbili. Je hawa wa madaraja ya chini watapigwa flatrate au kutakuwa na madaraja ya ulipaji kodi? Nadhani mtakuwa mnajua saluni ghali za kike na kiume. Kuna barber shop ukiingia utadhani umeingia kwenye mall fulani hivi! kunaye hadi air condition na macosmetic ya kila aina
 
Mifumo inasomana, ina maana ukisajiliwa BASATA, TRA watasoma nao watakuja kutaka chao, BRELLA nao watataka chao, wengine wenye mamlaka nao watataka chao. Hiyo hela ya kuchukuliwa na kila mamlaka itapatikana vipi nawe ubakishe za kuendesha maisha?
 
Hakika Watanzania wafundishwe kuwajibika kulipa kodi
Shida sio kulipa kodi. Tatizo linakuja kwenye matumizi. Wewe unahenyeka, wenzako wana budget ya kununua gari za mil 400.

Mazingira yangekua huru na haki, tungesema tunaweza gombea kupata huo ulaji wa keki ya taifa. Lakini nako wamebana waankula kwa kujuana.

Sijui kama umenielewa
 
Sasa hiyo inakuwa ni kodi ya kichwa.

Kama kodi si wanalipa kupitia Saluni zao wanazofanyia kazi?

Mwisho mtasema mpaka wacheza kamari tuwe tunalipa kodi.
Wanakamalia mbona wanalipa , kupitia mikeka yao ,badala ya kubuni namna ya kupunguza umaskini ,inabuniwa namna ya kuongeza umaskini. Hii haikubaliki, hawa watu huko kwenye maeneo yao wanalipa ushuru pia , aisee
 
Hii imekuja baada ya yule jamaa kusema anasafisha kucha kwa laki 5 kwa kila kichwa kimoja na ana wateja kibao huko masaki
Hahahaha Kuna pia yule winga alisemaga anaingiza milioni moja kwa siku, unamkumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…