Waswahili wanasema : "Kuuliza si ujinga"

Waswahili wanasema : "Kuuliza si ujinga"

Chifu mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2025
Posts
422
Reaction score
489
Habari za jioni mabibi na mabwana.
Kama kichwa cha habari kinavyosema kuuliza si ujinga!
Mimi ni muislamu ila hupenda kujua pia habari za watu wa dini nyingine!
Swali langu ni kama ifuatavyo:
1️⃣ Je kwaresma ipo kwa madhehebu yote ya kikristo / kikristu au ni special kwa wakatoliki peke yao?
2️⃣ Je makanisa au madhehebu yote yanayoadhimisha kwaresma ni lazima kujichora misalaba myeusi kwenye mapaji ya uso au hili ni kwa wakatoliki peke yao?
Nauliza hivi kwa sababu siku moja nilikuwa naongea na dada mmoja msabato akasema kwenye usabato hawana sikukuu ya krismas wala pasaka ila sikukumbuka kumuuliza kuhusu kwaresma kama kwenye usababato ipo au haipo?!
 
Back
Top Bottom