Hivyo hivyo ni vigumu sana watu milioni 60 kuwaaminisha CCM haifanyi kitu ili wakubali kumkabidhi madaraka Mbowe aliyejinasibu ukabila na ubwanyeye, au Tundu Lissu aliyejinasibu matusi na usaliti, tens yuko nje ya Nchi.
Kura wakishindwa wanadai polisi wanawapiga, kwa nini wawapige? Hata kama unapigwa, kura zako si ziko pale pale?
Mwaka 2020 aligombea Urais akapata 13% Magu akapa 87%. Walipiga kura kwa kuona Bwawa la Nyerere, kuhamia Dodoma, kufufuka ATC, flyovers kila mahali, kutetea makanikia yetu, amani na utulivu, discine kazini, nk. Mr. Tundu alitaka wampe kura kwa kitu gani alichofanya? Hata hao 13% sidhani kama ni kweli au ni wendawazimu.
Hata wabunge walishindwa, hatukuona polisi kwa Sugu au Peter Msigwa au Halima au hata kwa Mbowe mwenyewe Wilayani Hai. Majimbo ya Arusha Mjini (Lema) au Rombo (Joseph 30) kote walianguka mchana kweupe, hata kwao wamewachoka.
Ni vigumu sana watu milioni 60 wakubali kuonja sumu kwa ushabiki tu. Tume tunayo, Katiba tunayo, kama wanataka waweke zao zavushoga na uraiapacha, waziweke kwenye Ilani zao kwanza.
Wanasema watafanya vurugu kuzuia Uchaguzi, ngoja tusubiri. Ila watoto wao na mke wake kumbe ni Raia wa Marekani hawatokuwepo kushiriki mikikimikiki kuvuruga uchaguzi 2025.
Sioni watapitia wapi lakini tunawasubirini.