Wataala wa Geography nahitaji ufafanuzi hapa!

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
Tumekua tukifundishwa toka primary kuwa mwaka mrefu una jumla ya siku 366 na ule mfupi una siku 365 na robo(1/4).

Sina shida katika mwaka mrefu, tatizo naliona hapo kwenye mwaka mfupi, siku 365 na robo. Hiyo robo siku inakuaje? Maana maisha yangu yote mpaka leo hii sijawahi kuiona hiyo robo siku.

NAOMBENI UFAFANUZI TAFADHALI.
 
Mwaka mdogo = 365!
Mwaka mkubwa =366!
...
Mzunguko wa kuesabu ni miaka minne = mitatu midogo na m1 mkubwa!
...
Katika huo m1 mkubwa kati ya hiyo mi4 toa siku moja, hapo utapata mwaka = siku 365 na ile siku moja iliyobaki ukiigawa kwa 4 ndio unapata robo!
...
Therefore, one year = siku 365 na robo!
 
Siku,masaa,dakika,sekunde ni vipimo vya muda

Hiyo robo ina maanisha masaa 6
 
Rudi katika maandiko ya biblia wakati wana wa Israel wakitoka utumwani kwenda katka nchi ya ahadi,pamoja na matatizo waliyoyapata walipigina vita na majeshi ya Misri,sasa kuna wakati Joshua alimwomba Mungu asimamishe jua kwa muda ili aweze kuyamaliza majeshi ya Misri hii ni kutokana na mashambulio aliyoyafanya yalikuwa yanaenda kuleta ushindi ila usiku ulikuwa unaingia kwa hiyo wasingeweza kuendelea kupigana kutokana na teknolojia ya wakati ule hivyo Musa alimwomba Mungu asimamishe jua lisizame kwa muda ili aweze kuwapiga wanajeshi wa Misri kwa wakati ule,inasemakana Mungu alisikiliza maombi ya Musa na alisimamisha jua kwa muda wa masaa sita,kwa hiyo wataalamu wa muda wanachukua hiyo kama rejea ya kupata robo siku kwani tofauti hiyo haijakuwa na mbadala hadi leo
NB:nimechanganya kati ya Musa na Joshua ni yupi aliyeomba muda lakini usahii ni
 
Hujui maths ndio shida lakini kariculation ukifanya vzr utaona siku inaisha saa 6 usiku ma .ck 1 ina masaa 24 nusu 12 robo siku 4 ukiangalia vizuri utagudua robo inapatikama kutoka kwenye hayo na masaa na ina be drived from mwez feb katoka mwaka husika kama hukaelewa nipigie cm nikufundishe vzr
 
Hili swali sio jepesi, nimepitia maoni yote lakini nahisi kama ulikuwa unataka kugusa kitu fulani muhimu, hata hivyo bado sijaelewa. Kama hiyo robo tunaitumia kila mwaka (saa sita usiku ya mwaka mpya) kwa nini kuna accumulation ambazo zinafanya siku nzima kila baada ya miaka 4 na kutengeneza tarehe 29 feb? Kwanza sioni kama kweli kuna robo siku tunaiacha au kuitumia, kwa sababu siku inaanza saa 6 kamili usiku na kuisha saa 5 na dakika 59 usiku, tangu tarehe 1-January mpaka tarehe 31 December (masaa 8760 ya mwaka mfupi). Hiyo robo iko wapi? Unataka kuniambia kuwa mwaka mfupi ulitakiwa kuwa na masaa (8760+ or - 6), kama ni hivyo mwaka mpya ungekuwa saa 12 asubuhi au saa 12 jioni

Kwa nini hiyo robo haipo kwenye mwaka mrefu? Maana mwaka tunaanza muda ule ule wa saa 6 kamili usiku. Nakubali kuwa itakuwa siku 366 kwa sababu ya tarehe 29 Feb, je robo iko wapi kama miaka mingine?

Please msaada, inaweza kuwa ngumu kunielewa.....
 
Tumekua tukifundishwa toka primary kuwa mwaka mrefu una jumla ya siku 366 na ule mfupi una siku 365 na robo(1/4).

Sina shida katika mwaka mrefu, tatizo naliona hapo kwenye mwaka mfupi, siku 365 na robo. Hiyo robo siku inakuaje? Maana maisha yangu yote mpaka leo hii sijawahi kuiona hiyo robo siku.

NAOMBENI UFAFANUZI TAFADHALI.

Ka swali kazuri haka
 
Ndio vitu tunatakiwa tuwe tunaelimishana huu Mtandaoni.
 
kwel kabsa,maana mfano mie nliambuliaga ka A cha geography necta, ila hata sielewag huo mwaka mrfu na mfup unakuaje!
 
Tumekua tukifundishwa toka primary kuwa mwaka mrefu una jumla ya siku 366 na ule mfupi una siku 365 na robo(1/4).

Sina shida katika mwaka mrefu, tatizo naliona hapo kwenye mwaka mfupi, siku 365 na robo. Hiyo robo siku inakuaje? Maana maisha yangu yote mpaka leo hii sijawahi kuiona hiyo robo siku.

NAOMBENI UFAFANUZI TAFADHALI.

Hapo kwenye bold hapako sahihi ndiyo m aana unapata shida. Mwaka wowote una siku 365 na robo basi. Sasa ili kurahisisha mahesabu robo zinaachwa kwa miaka mitatu (tunasema miaka mifupi baada ya kuiibia robo siku) na robo hizo zinawekwa kwenye mwaka wa nne ambao tunaita mrefu kwa vile sasa unakuwa na siku 366 kamili.
 
Ni kwamba si kweli kusema eti siku ina masaa 24, kuna muda kidogo unabaki..ni kiasi kidogo sana cha muda ambacho kikikusanywa kwa mwaka mzima tunapata masaa sita au robo siku..
ndio maana mwaka wa kawaida una siku 365 na robo na hiyo robo ikikusanywa kwa miaka minne tunapata siku moja na kutengeneza mwaka mrefu wa siku 366 yaani mwezi wa pili unakua na siku 29.
 
Hapo kwenye bold hapako sahihi ndiyo m aana unapata shida. Mwaka wowote una siku 365 na robo basi. Sasa ili kurahisisha mahesabu robo zinaachwa kwa miaka mitatu (tunasema miaka mifupi baada ya kuiibia robo siku) na robo hizo zinawekwa kwenye mwaka wa nne ambao tunaita mrefu kwa vile sasa unakuwa na siku 366 kamili.

Lengo la msingi ilikuwa ni nini? what wrong kama kila mwaka ungebaki na robo yake yaani masaa 8772? Tell me the logic
 
Mkuu hili swali lako ni jepesi sana endapo mchoro ukitumika.

Hata hivyo ngoja nitumie maelezo machache na mahali usipoelewa utauliza.

Labda tuanze na tafsiri ya neno mwaka, mwaka mmoja ni muda ambao dunia inatumia kulizunguka jua ili kukamilisha mzunguko mmoja.

Pia siku ni muda ambao dunia hutumia kukamilisha mzunguko mmoja wa masaa 24 katika muhimili wake.

Ili kukamilisha mzunguko huu dunia hutumia takribani siku 365.25, uwepo wa hiyo robo ya siku wala usikuchanganye kwa kuwa ni makadirio tu ya muda uliotumika mwaka sio kizio cha muda.

Hizi robo siku hutimia na kuwa siku moja kila baada ya utimilifu wa miaka minne, yaani robo zikijilimbikiza na kutimia nne ndipo hukamilisha hiyo siku moja ya ziada na kuwa mwaka wenye siku 366.
 
Mkuu jaribu kutofautisha kati ya earth's rotation na earth's revolution...

Kufanya complete revolution dunia uhitaji muda wa siku 365, masaa 5, dakika 46 na sekunde 12.

Huu ni muda sawasawa kabisa na muda tunaoweza kuumithilisha na siku ambazo ndege ya KLM inahitaji kusafiri kutoka Dar kwenda New York.

Au kwa kifupi huo muda ni mjumuiko wa muda(a total travel time) unaotumiwa na sayari dunia kusafiri kutoka point A(1st of January) within its eliptical path to point A again(this time inakuwa ni 31st of December).

Sasa huo muda ukiuhesabu kwa kutumia kifaa chochote chenye uwezo wa kuhesabu muda kwa mfumo wa siku, masaa, dakika, sekunde basi utapata muda ule niliouandika pale juu ambazo hukadiriwa kuwa siku 365.25

Hiyo robo huwa inaondolewa kwenye kalenda hii tuitumiayo ya Gregorian ili kuondoa mtafaruku wa majira ya mwaka, na hizo robo nne hujumlishwa kila baada ya miaka minne na siku hiyo huongezwa kwa kuitwa Februari ya 29.

Muda huu wa siku 365.25 au 366 hauna uhusiano wowote na hizi habari za mchana na usiku ziletwazo na rotation ya dunia ambayo ni effect nyingine kabisa.

Hili swali sio jepesi, nimepitia maoni yote lakini nahisi kama ulikuwa unataka kugusa kitu fulani muhimu, hata hivyo bado sijaelewa. Kama hiyo robo tunaitumia kila mwaka (saa sita usiku ya mwaka mpya) kwa nini kuna accumulation ambazo zinafanya siku nzima kila baada ya miaka 4 na kutengeneza tarehe 29 feb? Kwanza sioni kama kweli kuna robo siku tunaiacha au kuitumia, kwa sababu siku inaanza saa 6 kamili usiku na kuisha saa 5 na dakika 59 usiku, tangu tarehe 1-January mpaka tarehe 31 December (masaa 8760 ya mwaka mfupi). Hiyo robo iko wapi? Unataka kuniambia kuwa mwaka mfupi ulitakiwa kuwa na masaa (8760+ or - 6), kama ni hivyo mwaka mpya ungekuwa saa 12 asubuhi au saa 12 jioni

Kwa nini hiyo robo haipo kwenye mwaka mrefu? Maana mwaka tunaanza muda ule ule wa saa 6 kamili usiku. Nakubali kuwa itakuwa siku 366 kwa sababu ya tarehe 29 Feb, je robo iko wapi kama miaka mingine?

Please msaada, inaweza kuwa ngumu kunielewa.....
 
Mkuu jaribu kutofautisha kati ya earth's rotation na earth's revolution...

Kufanya complete revolution dunia uhitaji muda wa siku 365, masaa 5, dakika 46 na sekunde 12.

Huu ni muda sawasawa kabisa na muda tunaoweza kuumithilisha na siku ambazo ndege ya KLM inahitaji kusafiri kutoka Dar kwenda New York.

Au kwa kifupi huo muda ni mjumuiko wa muda(a total travel time) unaotumiwa na sayari dunia kusafiri kutoka point A(1st of January) within its eliptical path to point A again(this time inakuwa ni 31st of December).

Haina uhusiano wowote na hizi habari za mchana na usiku ziletwazo na rotation ya dunia ambayo ni effect nyingine kabisa.

Uko sahihi sana tu, mimi sijachanganya habari hata kidogo, tumia muda kidogo kuelewa hoja yangu. Hizo siku 365 na masaa 5, dakika 46 na sekunde 12 ni sawa na hayo masaa (8760 + 6). Ambapo kwa maelezo yako ni kutoka 1st January to 31st December. Swali ni je, kama hiyo 6 hrs (approximated masaa 5, dakika 46 na sekunde 12) tunatumia kila mwaka inawezekanaje ku-accumulate to 1 day after 4 years? Ila tayari nimepata jibu kutoka kwa pmwasyoke
 
Lengo la msingi ilikuwa ni nini? what wrong kama kila mwaka ungebaki na robo yake yaani masaa 8772? Tell me the logic

Mkuu - kama nilivoonyesha kwenye post ya awali, lengo ni kurahisisha mambo. Hakuna kinachopotea kwa urahissaji huo.
 
Back
Top Bottom