Timu ya Wataalamu wa Afya ngazi ya Wizara, Mkoa, Wilaya na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeingia mtaani na kufanya zoezi la upimaji sampuli za maji katika Visima, Mabwawa na Kaya pamoja na utoaji wa Elimu Wilayani Itilima Mkoani Simiyu.
Taarifa ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu imesema Elimu imetolewa kwa kila Kaya kwa Wananchi Wilayani Itilima ikiwa ni jitihada endelevu za Serikali pamoja na Shirika la Afya Duniani katika kukabiliana na Ugonjwa wa kipindupindu Mkoani Simiyu.