Wataalam wa aina za magari please

Wataalam wa aina za magari please

Chemwali

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
397
Reaction score
178
Naomba ushauri kati ya Toyota Estima na na Toyota Platz ipi gari ya nzuri ,imara kidogo kwa kununua?

1594804070405.png

Toyota Estima

1594804159968.png

Toyota Platz
 
Wasubirie wataalamu wa hizo kitu watakuja, Ila kwa mtazamo wangu hakuna Gari nzuri hapo!! Embu badili mawazo hamia kwenye IST, Carina Ti au hata RAUM new model ziko poa sana mkuu.
 
naomba ushauri kati ya Toyota Estima na na Toyota Platz ipi gari ya nzuri ,imara kidogo kwa kununua?

... Inategemea' ni kwa ajili ya matumizi gani, na pia budget yako, mazingira unayoishi (ubora wa barabara), kipato chako (nina maana matumizi ya mafuta)
 
Wasubirie wataalamu wa hizo kitu watakuja,,Ila kwa mtazamo wangu hakuna Gari nzuri hapo!! Embu badili mawazo hamia kwenye IST,Carina Ti,au hata RAUM new model ziko poa sana mkuu.

Toyota CAMI na Vitz je? Nipe mtazamo wako!
 
... Inategemea' ni kwa ajili ya matumizi gani, na pia budget yako, mazingira unayoishi (ubora wa barabara), kipato chako (nina maana matumizi ya mafuta)

Kabisa Mkuu !
 
Habari za jioni wakuu,

Naombeni msaada ninunue gari gani kati ya Honda Fit na Mazda Demio. Mimi si mtaalam sana ila hizi ni kati gari ambazo naona si ghali sana na matumizi ya mafuta pia si makubwa.

Matumizi yangu ni kwaajili ya safari za mjini ofsin na shamba siku mojamoja

Asanteni
 
I will go for Vitz,,Hata CAMI pia ni nzuri kama unakoishi barabara hazijakaa vizuri (between CAMI n VITZ the choice is your's mkuu)

Thx, kutokana na hali yangu ... I admire those two brand, as nategemea kuanza maisha ya familia, naAMI ... thx anyway...
 
Habari za jioni wakuu,
Naombeni msaada ninunue gari gani kati ya Honda Fit na Mazda Demio. Mimi si mtaalam sana ila hizi ni kati gari ambazo naona si ghali sana na matumizi ya mafuta pia si makubwa.

Matumizi yangu ni kwaajili ya safari za mjini ofsin na shamba siku mojamoja

Asanteni

Mazda kimeo Ikiharibika mpaka upate kifaa utasahau hata jinsi ya kupiga starter.
 
Vipi kuhusu Nadia jamani mnaionaje, ya 2000, naomba msaada nakaa maeneo ambayo lami ni eneo kubwa mara chache sana barabara ya vumbi huko ukweni.
 
Habari za jioni wakuu,
Naombeni msaada ninunue gari gani kati ya Honda Fit na Mazda Demio
Mimi si mtaalam sana ila hizi ni kati gari ambazo naona si ghali sana na matumizi ya mafuta pia si makubwa
Matumizi yangu ni kwaajili ya safari za mjini ofsin na shamba siku mojamoja
asanteni

So far sijasikia complain ya Honda Fit,bt Mazda Demio huwa zinasumbua Crank Shaft.so itoe mawazoni hiyo!look for Vitz,IST na Cami pia,sio magari mabaya!
 
Habari za jioni wakuu,
Naombeni msaada ninunue gari gani kati ya Honda Fit na Mazda Demio
Mimi si mtaalam sana ila hizi ni kati gari ambazo naona si ghali sana na matumizi ya mafuta pia si makubwa
Matumizi yangu ni kwaajili ya safari za mjini ofsin na shamba siku mojamoja
asanteni

Hizo gari zote ulizotaja yaani honda na mazda achana nazo zitakusumbua sana spare hasa kwa tanzania . Pia mafundi wengi zinawashinda . Na wengi waliowahi kuwa na magari hayo yamewahia wameyapati.

Na ndio maana hata kwenye mtandao unaona zikiwa used bei yake ni nafuu coz hazina soko. So futa mawazo hayo zitakusumbua. Nakushauri tafuta gari yeyote lakini iwe toyota.
 
naomba ushauri kati ya Toyota Estima na na Toyota Platz ipi gari ya nzuri ,imara kidogo kwa kununua?

Gari aina ya toyota huwa hazina matatizo makubwa na hasa upatikanaji wa spare kwa hapa tanzania ni rahisi. Ila nakushari kabla ya kununua angalia na cc za engine zisiwe kubwa sana.

At least cc ziwe chini ya 1800 kutokana na ulaji wa mafuta. Pia angalia na aina ya engine kama utapata za aina ya VVT-I au 4E ni nzuri zaidi.
 
Hizo gari zote ulizotaja yaani honda na mazda achana nazo zitakusumbua sana spare hasa kwa tanzania . Pia mafundi wengi zinawashinda .

Na wengi waliowahi kuwa na magari hayo yamewahia wameyapati. Na ndio maana hata kwenye mtandao unaona zikiwa used bei yake ni nafuu coz hazina soko. So futa mawazo hayo zitakusumbua. Nakushauri tafuta gari yeyote lakini iwe toyota.

Nakushukuru sana mkuu
 
Back
Top Bottom