Wataalam wa gonjwa la HIV, tujuzeni kama kuna ukweli juu ya jambo hili

John mungo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2013
Posts
1,008
Reaction score
1,028
Habari za Jumapili,

Kuna mtu alikuwa anamsafirisha mgonjwa ambae tayari alikua Mwathirika wa VVU. Sasa kwa bahati mbaya gari likapata ajali na wote kuumia vibaya kiasi cha kuvuja damu nyingi.

Sasa baada ya kutoa msaada kwa majeruhi na kukimbizwa hospital sasa, kuna kijana aliumizwa na bati katika pilika za uokozi na akawa amepata jeraha na aligusa zile damu za majeruhi.

Watu wakaanza kusikitika kuwa jamaa atakuwa ameathirika. Ila wakati tunajadili juu ya hilo, kuna dada mmoja akamweleza yule jamaa kuwa aende hospital ya Serikali, aende kitengo cha UKIMWI kabla ya masaa 72 atapatiwa dawa ya kukinga virusi kwa njia ya sindano na inaitwa PEP, hataathirika.

Sasa Madokta naomba mtufahamishe kuwa; Je, hiyo sindano ipo? Na ni kweli mtu ukiwahi kupata kinga hiyo ndani ya masaa 72 kuna uwezekano wa kupona?

Tafadhali Madokta tujuzeni nasi tujue jambo hilo kama lipo kweli.

Siku njema.
 
Ni kweli hiyo inaitwa PEP yaani Post Exposure Prophylaxis na inatolewa ndani ya masaa 72. Ila SI KWELI kwamba ni SINDANO. Ni Vidonge tu kama vile vya kupunguza makali y virusi. Na kwa kuwa hiyo ni high risk basi at apatiwe dawa zinaitwa (Zidovudine+Lamivudine+ Efavirenz) Ambapo atatumia kwa muda wa wiki 4 yaani mwezi mmoja. Naomba kuwasilisha.
 
Wahi hospital zipo dawa za kuondoa uwezekano wa kuambukizwa HIV.
 

Hongera kwa kunifumbua macho Nashukuru .

JUMA PILI NJEMA.
 

now ni TLE
 
now ni TLE

Yes Mkuu japo hii kitu bado haijaiingizwa rasmi kwenye guideline ya NACP ya 2012 maana ndiyo inayotumika mpaka sasa. Though kuja circular ambayo nasikia imetoka japo binafsi sijaiona. I hope kuondoa mkanganyio huu hiyo reviewed guideline ikitoka itakuwa poa sana.
 

Samahani naamini unaweza kunisaidia ufumbuzi kidogo katika hili swala. Kama ni jambo linalowezekana je kuna madhara gani mtu anaweza kupata let say kwa ajili ya kutumia hii kinga Mara nyingi mfano kila amalizapo kufanya ngono na mwanamke asie muamini
 
Mkuu resistance ndio kitu cha kwanza kitakachotokea. So haoshauriwi hivyo kabisaa.
 
Wataalam njoni jamani mtujuze ni jambo jema kufahamishana.
 
Hilo ni kweli,na ndo hua wanapatiwa hiyo tiba watu waliobakwa!
 
Samahani naamini unaweza kunisaidia ufumbuzi kidogo katika hili swala. Kama ni jambo linalowezekana je kuna madhara gani mtu anaweza kupata let say kwa ajili ya kutumia hii kinga Mara nyingi mfano kila amalizapo kufanya ngono na mwanamke asie muamini

Sasa itakua inatumika kimzaha...!
Bora ilivyokua haiwekwi wazi.
 
PEP ( Post Exposure Prophylaxis ) si dawa bali ni utaratibu wa kuwatibu watu ambao hawana VVU ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza wakawa wameambukizwa VVU kwa bahati mbaya.Njia ambazo mtu anaweza kupata VVU kwa bahati mbaya ni kama kubakwa, kugusa damu au maji maji kutoka kwa mgonjwa wa VVU wakati ukiwa na michubuko au ngono isiyo salama.Kabla ya kupewa tiba ni lazima upimwe VVU na ionekane kuwa hauna VVU tayari.Ili kinga ifanye kazi ni lazima upewe tiba ndani ya masaa 72 baada ya tukio.Dawa zinazotumika ni dawa zile wanazotumia wagonjwa wa VVU ila zinatolewa kwa muda wa mwez mmoja tu na ni za kumeza .
 
Ndio, dawa hiyo ipo. Baadhi ya wataalam wanasema inaweza kumkinga hata mtu aliyebakwa na mwenye VVU. Daktari flan alinambia kuwa ni rahisi sana kumkinga mtu aliyejichoma kwa bahat mbaya sindano yenye VVU kwani kuna dawa inafanya kazi ya km kuweka uzio/fensi (Kubound) sehemu husika na virusi havitaweza kusambaa na kwenda sehem nyingine ya mwili.

Japo ndo hivo haikingi kwa 100%. Nadhan ni kwa 80% au 75%. Wataalam watatusaidia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…