Wataalam wa kilimo tusaidieni kwa hili

Fundi mahiri wa ujenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2012
Posts
4,159
Reaction score
2,844
Kutokana na jua kali kipindi cha kiangazi huwa mbogamboga hazistawi vizuri pia kipindi cha mvua mbogamboga hazistawi vizuri kutokana na mvua nyingi.

Je, kunauwezekano wa kuezeka shamba unalolima mbogamboga ili kuepukana na hizo kero?
 
Kutokana na jua kali kipindi cha kiangazi huwa mbogamboga hazistawi vizuri pia kipindi cha mvua mbogamboga hazistawi vizuri kutokana na mvua nyingi.

Je, kunauwezekano wa kuezeka shamba unalolima mbogamboga ili kuepukana na hizo kero?

uwezekano upo mkuu...
hali ya jua Kali au mvua nyingi huweza kuathiri ukuaji wa mazao kama mboga mboga kwani mboga huhitaji tu kiasi fulani tu cha maji ili kukua vizuri..
Ili kuzuia hili greenhouse hutumika... green house huwa na special cover ilinaloweza kupitisha kiwango flani cha mwanga na kuzuia mvua na wadudu kuingia katika shamba ila umwagiliaji/irrigation huitajika katika greenhouse yako!!!
 

Jomla - amechangia wazo zuri kuhusu green house.

Kuna aina mbili za green house -
1. glass greenhouses
2. plastic greenhouses

Nchi za arabuni (middle-east) watumia zaidi plastic green house. Kilimo katita nchi hizi si rahisi kwa sababu ni joto sana na mvua sio nyingi, lakini wanazalisha mboga nzuri.

Kuna taratibu za utumiaji wa greenhouse.
Kama unaweza kusoma na kuelewa vizuri kiingera, jaribu ku-Google na utapata maelezo mazuri yaundani zaidi. Lakini kama lugha kutatanisha, basi usione aibu kuomba maelezo/tafsiri kwa kiswahili.

Kama kuna wana JF hapa ambao wanajua NGO ambazo zinawaelimisha wakulima, itakuwa vizuri wakufahamishe uende wapi ili ukaelimike vizuri.

Natumaini utapata unachokitafuta na kwa manufaa ya wengine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…