Wataalam wa magonjwa ya akili, tangu jana nyumbani hatulali kaka amechanyikiwa hivyo ni vurugu tu

Wataalam wa magonjwa ya akili, tangu jana nyumbani hatulali kaka amechanyikiwa hivyo ni vurugu tu

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,601
Reaction score
1,172
Kwanza kabisa niwape pole Kwa majukumu. Nina kaka yangu. Wa damu 1 niliemfuatia. Alianza na kulalamika kuwa mke wake anamsumbua lakini mwezi umepita akawa ni mkali hata kwa jambo dogo. Ongea yake ni ukali tu.

Lakini badae ikafika hatua na mkewe wakaachana yani akamfukuza kutokana na maelewano ndani ya nyumba. Wakagawana Mali zao Sasa tangu pale wiki 3 Sasa Hali ikazidi kuwa mbaya, hivi sasa tupo nae hospital tumefunga kamba asikimbie.. Wataalam wangu nisaidieni tatizo ni nini hasa? Ili kaka awe kama mwanzo ushauri wenu wadau.

Asanteni.
 
Wataalamu halisi wa magonjwa ya akili wamekatazwa kuagua magonjwa kwa kupitia maelezo hafifu ya kwenye internet.

Huwezi kusikia mtu kama Prof. Kilonzo anaagua magonjwa ya akili kwa kusoma habari kwenye forum, kufanya hivyo ni kuvunja miiko ya taaluma. Ukiona daktari anaagua hivyo ujue kajanja huyo, si daktari aliyejua miiko ya kazi.

Huko Hospitali hakuna wataalamu waliomuona na kumkagua vizuri?
 
Poleni kwa kuuguza, kama mgonjwa yupo hospitali ni vizuri kwani kuna mabingwa huko wataweza kumpatia matibabu, kama ndiyo ikishindikana basi hapo unaweza kupata wataalamu wa tiba mbadala.
Lakini kuweni na subira Mungu akipenda atarudi kama zamani.
 
Nashukuru sana mkuu
 
Pole sana Mkuu, jaribu pia kwenda ktk ulimwengu wa roho yaani katika dini itasaidia.

Napendeza mkuu na yeye apelekwe hospitalini maana akili zake zimeruka naye (jokes)
 
Wataalamu halisi wa magonjwa ya akili wamekatazwa kuagua magonjwa kwa kupitia maelezo hafifu ya kwenye internet.

Huwezi kusikia mtu kama Prof. Kilonzo anaagua magonjwa ya akili kwa kusoma habari kwenye forum, kufanya hivyo ni kuvunja miiko ya taaluma. Ukiona daktari anaagua hivyo ujue kajanja huyo, si daktari aliyejua miiko ya kazi.

Huko Hospitali hakuna wataalamu waliomuona na kumkagua vizuri?
ungetuliza akili,ungeweza kutoa ushauri mzuri wenye faraja kwa mleta mada zaidi ya hii porojo uliyoandika.
 
Pole sana ndugu '
Hiyo hali inawakuta watu wengi japo kiwango hutofautiana hata kwa wale wanaopoteza wachumba ,mali ,kazi na n.k

>ila tukirudi katk swala la ndugu yako kuwa hilo ni tatzo kwake limekuwa kubwa na ameshindwa kulikabili pamoja na nyie mlichukulia kuacha na mke wake ni jambo jepesi sasa ipo hivi

>ndugu yako amekubwa na Msongo wa mawazo ambao umempelekea depression na mkakanyiko wa akili [ukichaa] hali imesababisha na mawazo ya muda mrefu ambayo amechelewa kufanya maamuzi kamili [yaan alimua kumuacha ila akili ilikuwa hajajikamilisha kumuacha kimamilifu] incomplete decision

>Amekuwa na wakati wakufikiria malengo alieweka na kujipanga wakat wote na huyo mwanamke [ameshindwa kuyapotezea na kukubali hali yake ya sasa na kuanza upya ]
Ushauri kwa ujumla kwa Ndugu yako akikubwa na matatzo kama hayo usione kawaida atakama yupo kawaida mambo yakufanya
>kuwa nae karbu sana muda mwingi
>muuache akuulezee hisia zake na machungu yake
>muache alie alie kbisa [usimkatize kuulza maana kulia humsaidia kupunguza homon za uzuni iliyoingia katk damu) na kumpa unafuu
>muache aongee yeye kuliko wew
>mpeleke mazingira mapya
>usiku lala nae au mpe vidonge vya usingizi [ila kuna vidonge maalumu nenda hospital watatoa].
>ajihusishe na ngono salama kwa MTU mwingine kadiri awezavyo
>muongoze kufanya mazoezi
>mpeleke kwa wataalumu wa saikolojia.
 
Nashukuru sana mkuu umenipa kitu nilichokua natarajia japo wengi hawakugundua nilichokua nakihitaji.. Nina swali kidogo Mara nyingi tiba zake ni za dawa zaidi au nijikite Sana na counseling?
 
ungetuliza akili,ungeweza kutoa ushauri mzuri wenye faraja kwa mleta mada zaidi ya hii porojo uliyoandika.
Wewe ambaye hujaeleza kwa nini na nilipokosea ni wapi hujatuliza akili zaidi yangu.
 
Mkuu huyo hajawai kukumbana na shida mwache tu
Umejuaje hilo? Au unaagua kwa mtandao tu?

Nendeni hospitali mkapate ushauri wa wataalam watakaopata nafasi ya kumtazama mgonjwa.

Hapa mtandaoni hakuna mtaalamu anayejua miiko ya taaluma anayeweza kukupa ushauri zaidi ya kukuambia nenda hospitali uonane na mtaalamu.

Wabongo wengi sana tuna tatizo la kupenda sana shortcuts.

Unataka mtu akueleze tatizo la mgonjwa ambaye hata kumuona hajamuona, tena kwa tatizo lililo so technical kama la akili.

Huyo mtu anayeshauri hata credentials zake hazijulikani, kamani a Profesa Ganga Ongo type of quack or whatever bush doctor wannabe out there.

Unatakakuwa desperate tu kuchukua ushauri.
 
Nashukuru sana mkuu umenipa kitu nilichokua natarajia japo wengi hawakugundua nilichokua nakihitaji.. Nina swali kidogo Mara nyingi tiba zake ni za dawa zaidi au nijikite Sana na counseling?
Inategemea MTU wako amefikia kiwango kipi ila kwakuwa nyie mlichelewesha sana naomba mufikishe hospital kabisa ili arejee kwenye hali yake mapema zAidi

Kwa level ya familia inabidi tuanze mjua MTU tangu tatzo limetokea na kumsaidia kwa ukarbu zaid
 
Kwanza kabisa niwape pole Kwa majukumu. Nina kaka yangu. Wa damu 1 niliemfuatia. Alianza na kulalamika kua mke wake anamsumbua lakini mwezi umepita akawa ni mkali hata Kwa jambo dogo. Ongea yake ni ukali tu. Lakini badae ikafika hatua na mkewe wakaachana yani akamfukuza kutokana na maelewano ndani ya nyumba. Wakagawana Mali zao Sasa tangu pale wiki 3 Sasa Hali ikazidi kua mbaya hivi Saivi tupo nae hospital tumefunga kamba asikimbie.. Wataalam wangu nisaidieni tatizo ni nini hasa? Ili kaka awe kama mwanzo ushauri wenu wadau. Asanteni.
UGONJWA WA KAKA YAKO TIBA YAKE NI UTATUZI WA MGOGORO NA MKE WAKE YAANI HAPO KIKUBWA NI MKE KUWA AU KURUDI TU HAKUNA TIBA NYNGINE. NA KAMA CHANZO CHA KUACHANA NI MWANAMKE KUMKATAA WAKATI ALIPENDWA AISEE TIBA NI HUYO WIFI YAKO TU...
 
Back
Top Bottom