habari wanajf hususani wanataaluma wa sheria tatizo langu linahusu mirathi kama ifuatavyo; mzazi wangu wa kiume alifariki 2009 alikuwa mwajiriwa wa serikali huko mwanza. Kikao cha ukoo kikamteua baba mdogo kuwa msimamizi wa mirathi,huyo baba mdogo alijaribu kufuatilia akianzia mahakama ya mwanzo kwa kule anakoishi(baba mdogo anaishi sehemu tofauti na alipokuwa akiishi baba yetu). Mahakama ya mwanzo wakamwambia aende wilayani,alikwenda kama mara mbili tu kisha hakwenda tena akidai hana nauli. Hivi majuzi sisi watoto tukaamua kumwita baba mdogo atuelezee kuwa amefikia wapi na akatuelezea kama jinsi nilivyoelezea hapo juu,na akadai kuwa jukumu hilo ananiachia mimi kwa sababu nimekua nifuatilie mwenyewe. Maswali yangu kwenu wanasheria ni kuwa, 1:je katika kuifungua kesi hiyo ya mirathi ni lazima nikafungulie kule alikokuwa anafanyia kazi marehemu au naweza kufungulia popote tanzania? 2: kama baba mdogo tayari alikuwa ameifungua kuna ulazima wa kurudi alikokuwa ameifungua au naweza kuanza tu upya?