Wataalam wa sheria saidieni hii issue

Wataalam wa sheria saidieni hii issue

Adm

Senior Member
Joined
Sep 19, 2010
Posts
149
Reaction score
45
habari wanajf hususani wanataaluma wa sheria tatizo langu linahusu mirathi kama ifuatavyo; mzazi wangu wa kiume alifariki 2009 alikuwa mwajiriwa wa serikali huko mwanza. Kikao cha ukoo kikamteua baba mdogo kuwa msimamizi wa mirathi,huyo baba mdogo alijaribu kufuatilia akianzia mahakama ya mwanzo kwa kule anakoishi(baba mdogo anaishi sehemu tofauti na alipokuwa akiishi baba yetu). Mahakama ya mwanzo wakamwambia aende wilayani,alikwenda kama mara mbili tu kisha hakwenda tena akidai hana nauli. Hivi majuzi sisi watoto tukaamua kumwita baba mdogo atuelezee kuwa amefikia wapi na akatuelezea kama jinsi nilivyoelezea hapo juu,na akadai kuwa jukumu hilo ananiachia mimi kwa sababu nimekua nifuatilie mwenyewe. Maswali yangu kwenu wanasheria ni kuwa, 1:je katika kuifungua kesi hiyo ya mirathi ni lazima nikafungulie kule alikokuwa anafanyia kazi marehemu au naweza kufungulia popote tanzania? 2: kama baba mdogo tayari alikuwa ameifungua kuna ulazima wa kurudi alikokuwa ameifungua au naweza kuanza tu upya?
 
DAH POLE MKUU yaani nimaswala magumu acha tuoni kama wataalam wana muda wakulipitia hili maana wame banwa na majukumu hata wanakosa kuandika miongozo kwa sie tusio ijua vema sheria
 
Sio lazima kwenda kufungulia huko ila ni vizuri kufungulia huko sababu hutapata shida ya kupata ushahidi na mashahidi wa baba yako endapo mirathi itakua complicated.
Ni vyema kama alishafungua kule ukamalizie huko huko. Jiulize vipi alipofungulia baba mdogo, then imefika point ya kupinga mirathi na akajitokeza mtu kupinga huku nyie mkiwa hamuonekani?
Otherwise uende huko shauri lilipofunguliwa ukajieleze vema the whole situation watakusaidia kukupa ushauri mzuri zaidi.
 
Dah,nimefuatilia madai yako naona kuna kitu sijakielewa.Iyo kesi ya mirathi ni zidi ya serikali au nyinyi wanandugu hamjaelewana kwenye mgao?maana umesema baba yako alikuwa mwajiriwa wa serikali.Labda nikushauri tu kwamba umtafute mwanasheria anaitwa Mr.Alloyce Komba huwa naona makala zake kuhusu sheria za mirathi kwenye gazeti la HABARI LEO jumapili.Mtafute atakusaidia.
alloycekomba@gmail.com
 
Sio lazima kwenda kufungulia huko ila ni vizuri kufungulia huko sababu hutapata shida ya kupata ushahidi na mashahidi wa baba yako endapo mirathi itakua complicated.
Ni vyema kama alishafungua kule ukamalizie huko huko. Jiulize vipi alipofungulia baba mdogo, then imefika point ya kupinga mirathi na akajitokeza mtu kupinga huku nyie mkiwa hamuonekani?
Otherwise uende huko shauri lilipofunguliwa ukajieleze vema the whole situation watakusaidia kukupa ushauri mzuri zaidi.
There you are!
Shauri linaweza kufunguliwa popote na mashahidi hawana budi kupatikana...hili ndilo linaupa umuhimu swala la kufunguliwa karibu na sehemu husika!!!!!
 
habari wanajf hususani wanataaluma wa sheria tatizo langu linahusu mirathi kama ifuatavyo; mzazi wangu wa kiume alifariki 2009 alikuwa mwajiriwa wa serikali huko mwanza. Kikao cha ukoo kikamteua baba mdogo kuwa msimamizi wa mirathi,huyo baba mdogo alijaribu kufuatilia akianzia mahakama ya mwanzo kwa kule anakoishi(baba mdogo anaishi sehemu tofauti na alipokuwa akiishi baba yetu). Mahakama ya mwanzo wakamwambia aende wilayani,alikwenda kama mara mbili tu kisha hakwenda tena akidai hana nauli. Hivi majuzi sisi watoto tukaamua kumwita baba mdogo atuelezee kuwa amefikia wapi na akatuelezea kama jinsi nilivyoelezea hapo juu,na akadai kuwa jukumu hilo ananiachia mimi kwa sababu nimekua nifuatilie mwenyewe. Maswali yangu kwenu wanasheria ni kuwa, 1:je katika kuifungua kesi hiyo ya mirathi ni lazima nikafungulie kule alikokuwa anafanyia kazi marehemu au naweza kufungulia popote tanzania? 2: kama baba mdogo tayari alikuwa ameifungua kuna ulazima wa kurudi alikokuwa ameifungua au naweza kuanza tu upya?
Ni vizuri ukaenda kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa (alipokuwa marehemu na wewe).

Hakikisha kimaandishi babayako mdogo, pamoja na ndugu zako (watoto wa Marehemu) wameridhia uwe msimamizi.

peleka barua mahakamani 9local magistrate) ufungue mirathi. utangaze katika gazeti la serikali mtu yeyote anayemdai au kudaiwa na marehemu ajitokeze within 45 days.

Zikipita, mahakama itakupa usimamizi wa mali za marehemu, na wewe uende serikalini na hati hiyo ya mahakama ili upate mafao.

Na kama una hati za mashamba au nyumba au fixed assets zinazoweza ingiliwa, make sure unawajulisha wenyekiti wa mtaa/kijiji kuwa wewe ndiye msimamizi na unawapa copy za maaamuzi ya mahakama.

kama shamba au kiwanja kimeingiliwa, ukionyesha papers za mirathi, basi hiyo ni mali yako mpaka aliyeingilia athibitishe mahakamani otherwise.
 
Back
Top Bottom