Wataalam wa sheria ya offside tunaomba ufafanuzi hapa

Sawa mkuu nakurudishia nyuma tena. hapa nakuwekea kipindi ambacho mpira unaenda kwa Morrison, angalia position ya Luis yupo wapi?View attachment 1722329
Kwa picha hii ni ngumu kujua, sababu mchukua picha hayuko usawa wa anaposimama kibendera, bali yuko nyuma kidogo.

Ila kwa kua mechi niliiona wacha nikujibu kama ifuatavyo. Goli hili ni Offside kwa Luis Jose Miqussoine, ilipaswa likataliwe.

Goli alilofunga Mugalu ni goli halali, ilipaswa likubaliwe. Hakukua na Offside kwa Mugalu wala aliepiga mpira kabla yake.

Mechi ya Yanga, goli alilofunga Fiston ni Offside, lilipaswa lilipaswa likataliwe.

Siwezi kusema kua marefa au vibendera wanapendelea bali ni udhaifu tu wa kibinadamu. Mechi ya Simba kibendera angeweza kua alikua anamuangalia zaidi Morrison akamsahau Miqussoine.

Yote ya yote Azam ni mdau mkubwa wa michezo hapa Tanzania. TFF wangeweza kua na muamuzi mmoja akakaa studio za Azam awe anawasiliana na Mwamuzi alieko uwanjan. Yaan kmaa "VAR" flani hivi.
 
Beki wawili wapo usawa wa Morison,uyu wa kushoto na yule wa kulia kwa mbaali akiangalia golini kwake.
BM kampa ubavu kipa,mpira umepigwa akiwa usawa wa mabeki.

Mpira umepigwa kutokea upande wa kulia ambapo BM anamuangalia mtoa assist.

Kumbukeni pia hali ya misimamo ya mabeki mshambiliaji pamoja na move ya mpira kwa pamoja vinatoa uhalisia wa off side.
Hapo hakuna off side.
Offside ipo, ila sio kwa Morrison, bali Miqussoine
 
Azam wana kipindi kila alhamisi kinaendeshwa na Othmani Kazi ambaye kitaaaluma alikuwa mwamuzi kinaitwa kipenga cha mwisho.
Alifanya uchambuzi wa matukio yote kuanzia penati, faulu na magoli yenye utata.
Mojawapo ya mechi alizochambua ni mwadui na azam, mechi ya kmc , yanga na coastal, yanga na polisi na simba na prisoni.
Mechi ya yanga na coastal kwa kupitia picha za marudio goli walilofunga yanga halikuwa halali kwani Kisinda alimsukuma mchezaji wa coastal kabla ya kufunga, goli la Fiston dhidi ya polisi pia halikuwa halali kwani mfungaji alikuwa ameotea kabisa pia hata kadi nyekundu aliyopewa Yondani haikuwa halali kwani yondani ndiye alianza kuchezewa rafu na mshika kibendera alikuwa eneo la tukio.
Mechi ya prison na simba kadi nyekundu ilikuwa halali kwani mchezaji wa prison alifanya faulu ya hatari.
Goli.la simba lililofungwa na mugalu lilikuwa halali lakini goli alilofunga konde boy halikuwa halali kwa sababu mfungaji aliotea.
Pia simba walinyimwa.penati ambayo Kapombe alishikwa mkono na hiyo ilitokana na uzembe wa mshika kibendera na uzembe wa mwamuzi kuwambali na tukio.
Nitajaribu kuleta huo uchambuzi ila ukienda youtube utaupata kupitia kipenga cha mwisho azam tv.
Tatizo la mtoa mada ni tatizo sugu la wanautopolo ambao var yao inaangalia sehemu moja tu pale inapokuwa na faida kwao kwa sababu kama maamuzi yamemkera alitakiwa kuangalia maamuzi ya pande zote na mechi zote ikiwamo ile ambayo wao walinufaika na maamuzi mabovu kama mechi ya coastal na mechi ya polisi tukiacha na mechi nyingine kama za kagera, gwambina na simba na kama maamuzi yangekuwa halali sasa hivi utopolo wangekuwa nafasi za katikati.
 
Tatizo umekariri, unadhani kila mtu yupo kama wewe ulivyo mpenzi/ mshabiki wa timu fulani. Sisi wengine ni wapenzi/ shabiki wa mpira hivyo mapenzi ya timu tunayaweka pembeni nakuzungumzia uhalisia wa jambo. Soma post namba 28 na 41 nilizungumzia goli la Kisinda na la Fiston kuwa hayakuwa halali
 
kama kukariri ni wewe uliyekariri kwani makosa ya yanga yalianza kabla ya mechi ya simba lakini hukutoa post yoyote kulalamika na hata ulipozungumzia goli la simba kuwa offside hukuzungumzia goli halali la simba lililokataliwa
 
Back
Top Bottom