Gari yangu aina ya toyota liteace ya dieseli ina toa muungurumo mbaya na kutoa moshi.
Pia taa ya check engine inawaka. Fundi wa kwanza akasema tumeweka mafuta machafu hivyo tusafishe tank. Fundi wa pili akasema tununue diesel treatment tuweke, na watatu akasema switch ya kwenye pampu ama pampu zenyewe zimekufa.
Katika hayo nilifanya yote isipokuwa pampu tu ila tatizo bado lipo vile vile. Nikaenda kufanya diagnosis na haya ndio majibu.
Nimechukua hii code na maelezo yake: "p1220" "timer control circuit malfunction"
Na kuweka google
Nimepata picha kadhaa, zinazo onyesha mahali tatizo lilipo.
Je nini cha kufanya?
- Tafuta fundi mwenye uzoefu na elimu, tumieni google kuweza ku_pin point ni kifaa kipi kinatakiwa kubadilishwa au kurekebishwa. Kila code ipo mtandaoni, ni swala la kutulia kwa muda ukifuatilia maelekezo yaliyopo. Hivyo itasaidia kufanya maamuzi ya hakika badala ya kubahatisha kama walivyofanya mafundi wa awali.