Kuhusu kufa nilikufaga mwaka 1492 ambapo nilikuwa naishi mtaa wa sumbaqha kijiji fulani kilichoko nchini Iran,
Nilikuwa nasumbuliwa kama huyu jamaa mara ya mwisho ikanitokea hiyo hali ghafla nikajikuta nipo mazingira mengine kabisa! Huwezi amini ilinichukua muda mrefu kuizoea ile hali.
Kuhusu shetani ni kwamba ule uovu tuufanyao ndio umetafsiriwa kama shetani..... Moto wa jehanam ni uongo tu mkuu ukifanya uovu hasara utayopata nikwamba kuna stage utashindwa kuvuka ambayo ni bora kuliko ya kibinadamu ndio maana na mimi nikazaliwa tena.
Tamaa yako usiiweke kwenye mwili ambao utauacha bali iweke kwenye kutafuta ukweli tu ili uvuke hiyo stage uingie iliyo bora zaidi.... Yaani kama game vile. Ukishindwa kuvuka unazaliwa tena. Maana utajikuta ukirandaranda ovyo na ndio utaanza kutaget mwili unakaribia kuzaliwa ili uingie uzaliwe upya😛