Wataalamu naomba msaada kwa haya mambo.

Wataalamu naomba msaada kwa haya mambo.

River Mbane

Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
27
Reaction score
4
1. Kuna matatizo inatokea mtu anakuwa na vimawe vidogovidoko katika figo zake na mara nyingi mtu huyo hufanyiwa upasuaji kuviondoa. Mimi ninachohitaji kujua ni hivyo vimawe vinaingiaje ktk mfumo wa damu hadi kufka kunako figo?Ninavyojua absorption inahusisha vitu vilivyo ktk ionic form e.g Na+ or in liquid form(end products of digestion) 2)Jana nimeenda hospital fulani kucheki afya yangu ktk vipimo vya mkojo niliambiwa mkojo wangu ni mchafu,sasa mimi nkajiuliza "kuna siku mkojo huwa unakuwa msafi?na ninavyojua mkojo ni takamwili"Nilijaribu kumuuliza doctor bt hakujali kunipa jibu hivyo nikaachana naye tu. I hope humu JF nitapata majibu sahihi
 
River Mbane,

Mawe mwilini huwa katika viungo mbalimbali, na huitwa kulikana na upatikanaji wa kiungo/viungo husika.

Mfano;
Cystolithiasis, Nephrolithiasis, Cystonephrolithiasis- Mawe katika mfumo wa mkojo.
Gallstones- Mawe katika mfuko wa nyongo.
Salivary gland/Prostate stones- Mawe katika tezi za mate, tezi dume.

Sababu mbalimbali husababisha tatizo hili kutegemeana na upatikanaji wa mawe yenyewe mwilini. Lakini katika kueleza/kujibu juu ya maswali yako,

Mkojo ni taka mwili, na ingawa ni taka mwili kuna kiwango cha USAFI katika mkojo huo huo mchafu, hapa ninamaanisha katika vipimo vya mkojo (Urinalysis, C/Sensitivity, etc) kuna kiwango maalum chenye kufanya ingawa mkojo ni mchafu kuwa kawaida (yaani taka mwili), na zaidi au juu ya kiwango hicho DALILI, au MADHARA mbalimbali yanaweza kujitokeza.

"Mkojo kuwa mchafu" imekuwa ikitumika kuonyesha wadudu katika mfumo wa mkojo!
Nini huleta tatizo hili;


Mawe katika mfumo wa mkojo!
Hii husababishwa na kujikusanya kwa 'kemikali/madini' ikiwa yakiwapo Calcium,Magnesium, phosphate n.k ambayo hutokana na sababu mbalimbali zikiwapo, kutokunywa maji kwa wingi (hii ikiwa ni sababu kuu), magonjwa mbalimbali ya mfumo huo, n k

Dalili:
Wengi wa wagonjwa (hutegemeana na upatikanaji wa mawe katika sehemu husika ya mfumo wa mkojo), huwa na maumivu ya tumbo, mgongo yanayoelekea sehemu za siri, maumivu wakati wa kukojoa, damu katika mkojo, kujisikia kukojoa mara kwa mara, kutapika na kuhisi kichefu chefu, n.k

Upimwaji, hujumuisha kupimwa mkojo ("usafi wake"), kuotesha wadudu, jupiga picha za tumbo (X-rays, na Ultra Sound Sonograghy, n.k)

Matibabu:
Iwapo shida ni mkojo mchafu pekee, tiba ya maji na dawa kulingana na ugonjwa wenyewe), endapo tatizo ni mawe katika mfumo huo, upasuaji na kuondolewa kwa mawe haya hufanywa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom