Wataalamu Umeme na Electronics, Msaada wenu hapa wa hiki ki redio

Wataalamu Umeme na Electronics, Msaada wenu hapa wa hiki ki redio

Baba Rhobi

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2020
Posts
1,611
Reaction score
2,881
Wakuu habari ya nyie, kuna hiki ki redio nimeombwa msaada hapa kukirekebisha, kina shida moja.

Waya ule wa speaker vile vidogo (Sijui ndo wanaviita twitter), pale kwenye ki tobo unapoingia kimekufa, sasa nafikilia hivi inawezakana nikauchukua na kuunga kwenye ule mwingine, tobo lililokufa ni la Right, ili zote mbili zipitiie left, sasa nawaza.

Hakuta kua na shida yoyote kufanya hivo.

Na je, Hilo tobo moja litaweza kusukuma hivyo vi Twitter viwili?

Picha hizi hapa kwa taarifa zaidi.

pia samahanini kwa Uandishi mbovu.

Chief-Mkwawa
dronedrake
 
IMG_20230821_194146_1.jpg
IMG_20230821_194500_1.jpg
IMG_20230821_194812_1.jpg
 
Huo waya kwenye hio picha ya mwisho ndo nafikilia kuunga kwenye huo mwingine.
Huo nilioshika na mkono hapo, nafikilia kuukata niunge kwenye huo wa left.
 
Kwa ninavyoelewa left na right ni kwa ajili ya Stereo, kutengeneza ile effect, ukitumia left tu ama right tu itakua ni Mono, vile vionjo vitapotea ila kazi itafanya. Jaribu utupe mrejesho mkuu.
Sawa mkuu, nashukuru mi hofu yangu ilikua kwamba hilo tobo moja linaweza shindwa kusukuma all two together.
 
nimekwepa hio stereo problem
effect za stereo zinakuja toka huko kwenye production, kama sauti haikuwekewa stereo effects basi hata utumie L na R itatoka Mono, na kama iliwekewa stereo basi kuziunga kwa njia moja zitapiga Mono

njia y L ina amplifier yake ndani ambayo itasukuma twitter ya MINIMUM Impedance X
njia ya R pia ina amplifier yake ndani pia ambayo itakusukuma impedance ile ile ya X

kama utaunga speaker zote 2 ( in parallel ) kwenye njia moja, na kama kila speaker ina impedance ya Y
ukiziunga in parallel (kwa kutumia hiyo splitter, na assume inaunga izo speakers in parallel mode/SAMBAMBA ) jumla ya impedance inakua Y/2

sheria ni kwamba hii Y/2 inabidi izidi impedance X tajwa ya hapo juu
 
Nashukuru sana mkuu.
 
Back
Top Bottom