Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa Corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MAELFU ya Wakenya wako katika hatari kubwa ya kufariki katika wimbi la tatu la Covid-19 kutokana na aina mpya ya virusi kutoka Uingereza, Afrika Kusini na Brazil.

Hatari hii inaongezeka zaidi kwa Wakenya kutokana na gharama za juu za matibabu katika hospitali za kibinafsi na huduma duni za afya ya umma nchini.

Pia wizi wa pesa za kukabiliana na Covid-19 mwaka 2020 kupitia KEMSA umeweka maisha ya Wakenya katika hatari kuu.

Hospitali nyingi zilizo na vitanda vya wagonjwa mahututi (ICU) zimeongeza bei kwa hadi mara tatu ya inayotozwa wanaougua maradhi mengine.

Uchunguzi wa Taifa Leo umeonyesha kuwa hospitali nyingi zinaitisha amana ya juu zaidi kabla ya mgonjwa wa Covid kukubaliwa kuingizwa ICU.

Hospitali za Nairobi Hospital na Mater jijini Nairobi zinatoza amana ya Sh600,000 huku ile ya kitaifa ya Kenyatta (KNH) ikidai Sh200,000.

Kulingana na daktari mmoja ambaye aliomba tusitaje jina lake, kuna baadhi ya hospitali jijini Nairobi zinazoitisha amana ya hadi Sh1 milioni.

Pesa hizi ni sehemu ya kwanza tu ya gharama, kwani zinaongezeka kwa Sh52,000 kila siku, ambayo ni ada za kuhudumia wagonjwa wa Covid walio ICU kulingana na mwongozo wa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu (KEMRI) iliyotolewa mwaka 2020.

“Hali ikiendelea hivi, ugonjwa huu utaua maelfu. Ebu jiulize ni Wakenya wangapi wanaoweza kulipa Sh1 milioni kupata kitanda cha ICU? Ikizingatiwa kasi na hatari ya maambukizi, maskini wengi, wakiwemo wahudumu wa afya wataangamia kwa wingi,” alisema daktari wa hospitali moja katika Kaunti ya Machakos aliyeomba tubane jina lake.

Hali imegeuka kuwa mbaya zaidi kutokana na uhaba wa vitanda vya ICU, ambapo asilimia 87 ya jumla ya 518 vilivyoko nchini kwa sasa vina wagonjwa.

Hii ina maana kuwa wengi wa wagonjwa ambao wamo katika hali mahututi wamo kwenye hatari ya kufariki kutokana na kushindwa kumudu gharama ya amana na ada za ICU, pamoja na kukosekana kwa vitanda hivyo.

Mashambani

Hii imetokea wakati ambapo maambukizi nchini yamefikia kiwango cha juu huku idadi ya wanaofariki nayo pia ikipanda.

Taasisi ya Matibabu ya Amerika (CDC) imeorodhesha Kenya katika ngazi ya nne, ambayo ina maana kuwa nchi imo na maambukizi ya kiwango cha juu zaidi.

Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya mashambani kutokana na huduma duni katika hospitali nyingi. Hii inawaacha wakazi wa mashambani, ambako umaskini uko juu zaidi, katika hatari zaidi ya kufariki kutokana na makali ya Covid-19.

Mnamo Jumatatu, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alionya kuwa kuwa hospitali zinalemewa na wagonjwa kufuatia wimbi la tatu la maambukizi ya corona.

Madaktari wanasema ukosefu wa vitanda vya wagonjwa mahututi na oksijeni katika hospitali za umma unasababisha vifo vya wagonjwa wengi wanaombukizwa virusi hivyo.

Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua.

Pia uhaba wa kemikali za kupima virusi vya Covid-19 una maana wengi hawajui wanaugua.

Hali hii imeibuka ikigunduliwa kuwa kaunti nyingi hazikuweka vitanda 300 kila moja katika maeneo ya kutenga wanaoambukizwa virusi vya corona kama zilivyoagizwa na Rais Uhuru Kenyatta mwaka 2020.

Pia imeibuka hospitali nyingi mashinani hazina vitanda vya ICU. Wiki iliyopita, mwanahabari katika Kaunti ya Embu aliyekuwa hali mahututi, alikosa kitanda na ikabidi apelekwe kaunti jirani ya Murang’a.

Madaktari nao wanahofia kuwa jinsi maambukizi yanavyoongezeka ndivyo nao wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa corona wakiwa kazini.

“Kila mtu yumo kwenye hatari. Hili wimbi la tatu ni hatari zaidi kwa sababu ya uhaba wa vifaa na vyumba vya kutibu na kutenga wagonjwa,” asema daktari katika KNH.

Hali hii inapotokea, watu waliofaidika na mabilioni ya pesa za kushughulikia janga la corona bado hawajachukuliwa hatua, licha ya Rais Uhuru Kenyatta mwaka 2020 kuagiza wakamatwe na washtakiwe.

Zaidi ya Sh7.6 bilioni zililipwa watu na kampuni zilizopata tenda ya kuuzia serikali vifaa vya kujikinga na corona kupitia Shirika la Kusambaza Dawa la Kenya (KEMSA).

Pia kuna hofu kwamba baadhi ya pesa zilipewa kaunti kujiandaa kukabili janga la corona zilitumiwa vibaya.
 
Nyingi wakenya mnafuata masharti ya kujikinga lakini mnaripoti Corona inapaa.bongo hakuna barakoa, sanitizer, hakuna kunawa mpaka wakati kula. Chunguzeni viongozi wetu wanataka kukopa Tena Kisha wafisadi.bongoland Corona ni kawaida sana haisumbui Kama malaria.tena kwa wanaopenda viyoyozi muda wote.

Wilayani kwetu kusini mwa bongo kiukweli hatujawahi poteza mtu kwa dalili za corona. Je, huko mpaka WILAYA za mbali na Nairobi Corona ipo.
 
Nyingi wakenya mnafuata masharti ya kujikinga lakini mnaripoti Corona inapaa.bongo hakuna barakoa, sanitizer.hakuna kunawa mpaka wakati kula.chunguzeni viongozi wetu wanataka kukopa Tena Kisha wafisadi.bongoland Corona ni kawaida sana haisumbui Kama malaria.tena kwa wanaopenda viyoyozi muda wote.
Wilayani kwetu kusini mwa bongo kiukweli hatujawahi poteza mtu kwa dalili za corona.je? huko mpaka WILAYA za mbali na Nairobi Corona ipo.
hebu cheki >>> Jukwaa la Siasa
 
Hizi jeuri zenu ndio zimesababisha mumetuzungusha siku kadhaa mkisema rais anapiga kazi yuko busy tu halafu ghafla mumeita dunia yote iomboleze na nyie na kuanza kuwasema ambao hawajaja akina Museveni na Kagame.
Endeleeni kukaidi na kujifanya makomando dhidi ya corona.....
Sisi huku tunachukua tahadhari na kila tukifa hatujidanganyi na huo ujuha wa changamoto la kupumua, muda huu wengi tunasubiri chanjo kwa hamu maana hatuna hizo hela ndefu za kulazwa Nairobi hospital.

Sema kuna baadhi yenu mumeanza kuwa na akili, huyu hapa kawapigisha nyungu hatimaye akili zimemuingia

2721819_Jafo.png

hqdefault.jpg
 
Maoni ya mtu binafsi kuhusu kutokuja kwao.afya ya hao viongozi ni muhimu Sana sasa ukizingatia ni washiriki katika kuua northern corridor SGR na hoima pipe tulieni home wakuu.hajazuiwa mtu kutumia barakoa Ila hiari yake,sanitizer pia.na ikiwa lazima Basi inaondoka kabisa .hakuna kudanganya ili mabeberu watukopshe tufisadi never.kununua barakoa au sanitizer navyo lazima loans za mabeberu Tena unabembeleza!Kuna tatizo
Nasisitiza nilipo hatuzika mgonjwa Corona wodi zilizoandaliwa ziko wazi.
Uko kenya WILAYA za mbali na Nairobi na Mombasa covid ipo mpaka washiriki kulipa mzigo wa madeni
Uganda wamechukua hatua Kama Kenya zimewasaidia hawaangaiki kukopa na uchaguzi walifanya mikutano Bob wine alipiga Kama kawa + maandamano..kulikoni jirani bepari.au miongoni mwa covid aid millionaire
View attachment 1733193
 
Kwa sasa hata barakoa haziwezi kuwalinda wakija maana mnavyojianika na kukusanyika na kubanana hamna namna mgeni anaweza kujilinda, hivyo hao wamefanya busara kususia na kutuma salamu kwa mbali.
Masuala ya bomba sioni unayaleta kwenye mjadala ya nini maana ile ni biashara, ni maslahi na haihusiani na ujuha wenu kwa corona. Uganda na Rwanda hao ni na mabepari kama sisi, huwa wanajua namna ya kutenganisha maslahi ya biashara na hizo pumba za kuitana ndugu. Hivyo miradi itaendelea tu, ila kwa sasa afya ya hao viongozi ni muhimu.
 
Hatuwezi kuacha mfumo wetu eti kwa sababu wazungu huko ulaya na bara amerika wanakufa Sana..hapo Kenya kinapowachapa kipindupindu wao wanafanya lockdown kwao.au ukimwi Kama Corona inaua kiasi hicho hapa TZ kingekuwa na maiti barabarani.
Hao viongozi wamebaki kwao na Kama kawa sababu zao,Kama unaamini wameacha kuja kwa akili hizo Chanjo ni za majaribio awajiamini au blood clot inawatsha.
Maana wazungu wenyewe wanamashaka nazo.
Nchi nyingi za kiafrika Covid 19 si tatizo kiasi hicho.hatuna misongamano.watu wengi vijana hali ya hewa joto inasadia.mamboi ya kuomba kukopa ni ufisadi.
Barakoa,nawa mikono Kaa mbalimbali.haviitaji kukopa au kuomba misaada nje ya nchi.
Je?huko covid19 imesambaa vijijini. 99.9% ya vijiji vya Tanzania hajui hili gonjwa likoje .hatutaki serikali ikope au kupiga magoti ya msaada dawa za majaribio.
 
Mfumo upi mnao nyie, ikiwa hata panadol, ARV mnategemea hao hao, chanjo zote hata za homa ya njano mnawategemea, hizo pumba za kunywa maji yaliyotiwa limau eti ndio dawa dhidi ya corona zimefanya muonekane kituko cha dunia. Kwa sasa nyie ndio mnaongoza kwa kupoteza viongozi duniani, halafu mnalalamika eti sijui akina ndugu wa wapi hawaji kwenye misiba yenu...pitia hii link uone mnachojifanyia Jukwaa la Siasa Sema kwa kujitia upofu hautaona chochote.
 
Huo ndiyo ukweli halisi Mkuu.
Hizi jeuri zenu ndio zimesababisha mumetuzungusha siku kadhaa mkisema rais anapiga kazi yuko busy tu halafu ghafla mumeita dunia yote iomboleze na nyie na kuanza kuwasema ambao hawajaja akina Museveni na Kagame.
Endeleeni kukaidi na kujifanya makomando dhidi ya corona.....
Sisi huku tunachukua tahadhari na kila tukifa hatujidanganyi na huo ujuha wa changamoto la kupumua, muda huu wengi tunasubiri chanjo kwa hamu maana hatuna hizo hela ndefu za kulazwa Nairobi hospital.

Sema kuna baadhi yenu mumeanza kuwa na akili, huyu hapa kawapigisha nyungu hatimaye akili zimemuingia

2721819_Jafo.png

hqdefault.jpg
 
Hivi bado mawimbi yanaendelea tu, au wazungu wanatafuta jinsi ya kutupiga pesa?
 
Back
Top Bottom