Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa Corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua

Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa Corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua

hata hajafa pia ni maigizo.

unaamini katika maigizo sana.

Hehehe!! Nakumbuka yale maigizo kwamba yuko busy hana muda wa kwenda sijui Kariokoo au Magomeni...hivi mbona huwa hamna hata aibu au hofu ya Mungu, mnaongopa tena msikitini.
Mbelgiji kawakomalia na kuwapumulia mgongoni mpaka mkaachia.....
 
Majirani mshafika Corona wimbi la tatu dah!!

Mpo faster wakati sisi hata wimbi la kwanza hatujalianza...
 
Hehehe!! Nakumbuka yale maigizo kwamba yuko busy hana muda wa kwenda sijui Kariokoo au Magomeni...hivi mbona huwa hamna hata aibu au hofu ya Mungu, mnaongopa tena msikitini.
Mbelgiji kawakomalia na kuwapumulia mgongoni mpaka mkaachia.....

ashindwe kuhangaika na maisha yake anatafuta ganda la ndizi atelezee nalo kama kick!!!!

yule ni traitor tu,ndio maana kautuliza huko ubergiji kwa washkaji zake,lakini ana wafuasi vinumbo kama wewe,hata akisema anapita kuwalamba vitako wanaitikia"ndio mtaalamu"
 
ashindwe kuhangaika na maisha yake anatafuta ganda la ndizi atelezee nalo kama kick!!!!

yule ni traitor tu,ndio maana kautuliza huko ubergiji kwa washkaji zake,lakini ana wafuasi vinumbo kama wewe,hata akisema anapita kuwalamba vitako wanaitikia"ndio mtaalamu"

Kawapatia sana yule, kila anachoandika kinatimia, itakua anayo source ya ndani kwa ndani yenu hehehe, hayo marisasi mlimpiga naona hajawahi kupunguza hamaki maana maneno yanayomtoka...ama kwa kweli bora hivyo hakupewa urais maana nahisi angelipiza kisasi.
Kwa sasa ingekua busara apunguze hamaki.
 
Kawapatia sana yule, kila anachoandika kinatimia, itakua anayo source ya ndani kwa ndani yenu hehehe, hayo marisasi mlimpiga naona hajawahi kupunguza hamaki maana maneno yanayomtoka...ama kwa kweli bora hivyo hakupewa urais maana nahisi angelipiza kisasi.
Kwa sasa ingekua busara apunguze hamaki.

hawezi kuwa rais yule.

kwanza kwa hili alikofanya tu anaonekana wazi hajatosha kushika uongozi kama huo.
 
Gazeti lote hilo kumbe linaongelea hofu tu, kudhaniadhania tu, upuuzi mtupu! Badala ya kufanya tracer study kwa hao wagonjwa mliowapima na kuhakikisha kuwa wana corona ili kujiridhisha miisho yao! Mmeshaambiwa kuwa fatality late ni chini ya 2% afu unakuja na hofuhofu zako hapa, kafie mbali na hofuhofu zako! Tz tupo gado! Asante JPM! Rest in peace and power our hero🙏😭!
MAELFU ya Wakenya wako katika hatari kubwa ya kufariki katika wimbi la tatu la Covid-19 kutokana na aina mpya ya virusi kutoka Uingereza, Afrika Kusini na Brazil.

Hatari hii inaongezeka zaidi kwa Wakenya kutokana na gharama za juu za matibabu katika hospitali za kibinafsi na huduma duni za afya ya umma nchini.

Pia wizi wa pesa za kukabiliana na Covid-19 mwaka 2020 kupitia KEMSA umeweka maisha ya Wakenya katika hatari kuu.

Hospitali nyingi zilizo na vitanda vya wagonjwa mahututi (ICU) zimeongeza bei kwa hadi mara tatu ya inayotozwa wanaougua maradhi mengine.

Uchunguzi wa Taifa Leo umeonyesha kuwa hospitali nyingi zinaitisha amana ya juu zaidi kabla ya mgonjwa wa Covid kukubaliwa kuingizwa ICU.

Hospitali za Nairobi Hospital na Mater jijini Nairobi zinatoza amana ya Sh600,000 huku ile ya kitaifa ya Kenyatta (KNH) ikidai Sh200,000.

Kulingana na daktari mmoja ambaye aliomba tusitaje jina lake, kuna baadhi ya hospitali jijini Nairobi zinazoitisha amana ya hadi Sh1 milioni.

Pesa hizi ni sehemu ya kwanza tu ya gharama, kwani zinaongezeka kwa Sh52,000 kila siku, ambayo ni ada za kuhudumia wagonjwa wa Covid walio ICU kulingana na mwongozo wa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu (KEMRI) iliyotolewa mwaka 2020.

“Hali ikiendelea hivi, ugonjwa huu utaua maelfu. Ebu jiulize ni Wakenya wangapi wanaoweza kulipa Sh1 milioni kupata kitanda cha ICU? Ikizingatiwa kasi na hatari ya maambukizi, maskini wengi, wakiwemo wahudumu wa afya wataangamia kwa wingi,” alisema daktari wa hospitali moja katika Kaunti ya Machakos aliyeomba tubane jina lake.

Hali imegeuka kuwa mbaya zaidi kutokana na uhaba wa vitanda vya ICU, ambapo asilimia 87 ya jumla ya 518 vilivyoko nchini kwa sasa vina wagonjwa.

Hii ina maana kuwa wengi wa wagonjwa ambao wamo katika hali mahututi wamo kwenye hatari ya kufariki kutokana na kushindwa kumudu gharama ya amana na ada za ICU, pamoja na kukosekana kwa vitanda hivyo.

Mashambani

Hii imetokea wakati ambapo maambukizi nchini yamefikia kiwango cha juu huku idadi ya wanaofariki nayo pia ikipanda.

Taasisi ya Matibabu ya Amerika (CDC) imeorodhesha Kenya katika ngazi ya nne, ambayo ina maana kuwa nchi imo na maambukizi ya kiwango cha juu zaidi.

Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya mashambani kutokana na huduma duni katika hospitali nyingi. Hii inawaacha wakazi wa mashambani, ambako umaskini uko juu zaidi, katika hatari zaidi ya kufariki kutokana na makali ya Covid-19.

Mnamo Jumatatu, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alionya kuwa kuwa hospitali zinalemewa na wagonjwa kufuatia wimbi la tatu la maambukizi ya corona.

Madaktari wanasema ukosefu wa vitanda vya wagonjwa mahututi na oksijeni katika hospitali za umma unasababisha vifo vya wagonjwa wengi wanaombukizwa virusi hivyo.

Wataalamu wa afya wanahofia kuwa wagonjwa wengi wa corona wanafariki wakiwa nyumbani bila kujua wanaugua.

Pia uhaba wa kemikali za kupima virusi vya Covid-19 una maana wengi hawajui wanaugua.

Hali hii imeibuka ikigunduliwa kuwa kaunti nyingi hazikuweka vitanda 300 kila moja katika maeneo ya kutenga wanaoambukizwa virusi vya corona kama zilivyoagizwa na Rais Uhuru Kenyatta mwaka 2020.

Pia imeibuka hospitali nyingi mashinani hazina vitanda vya ICU. Wiki iliyopita, mwanahabari katika Kaunti ya Embu aliyekuwa hali mahututi, alikosa kitanda na ikabidi apelekwe kaunti jirani ya Murang’a.

Madaktari nao wanahofia kuwa jinsi maambukizi yanavyoongezeka ndivyo nao wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa corona wakiwa kazini.

“Kila mtu yumo kwenye hatari. Hili wimbi la tatu ni hatari zaidi kwa sababu ya uhaba wa vifaa na vyumba vya kutibu na kutenga wagonjwa,” asema daktari katika KNH.

Hali hii inapotokea, watu waliofaidika na mabilioni ya pesa za kushughulikia janga la corona bado hawajachukuliwa hatua, licha ya Rais Uhuru Kenyatta mwaka 2020 kuagiza wakamatwe na washtakiwe.

Zaidi ya Sh7.6 bilioni zililipwa watu na kampuni zilizopata tenda ya kuuzia serikali vifaa vya kujikinga na corona kupitia Shirika la Kusambaza Dawa la Kenya (KEMSA).

Pia kuna hofu kwamba baadhi ya pesa zilipewa kaunti kujiandaa kukabili janga la corona zilitumiwa vibaya.
 
Back
Top Bottom