Wataalamu wa Anatomy/Physiology saidieni hapa.

Carla

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
398
Reaction score
331
Kuna swali limetokea kunifikirisha sana, nalo ni hili:

Nini kinasababisha uvimbe/kuvimba(swelling). Ninahitaji kufahamu the process of swelling.
Najua zipo sababu nyingi za kuvimba, mfano kung'atwa na nyuki(mfano), kujigonga sehemu ya mwili, kuteguka kiungo fulani cha mwili n.k. Pia kuna sababu kama mtoki unaoweza kutokea sehemu mbalimbali. Wengine wataongezea sababu zao maana hata mimi nimeziacha nyingine.
Swali ni lile lile, nini kinatokea kwenye seli au tishu kinachopelekea uvimbe?
Karibuni.
 
The process of swelling comes as a result of cell injury and as the body defence itself, it release histamines as first line defence mechanism. As a result of this inflammation occurs and pain. Pain is also part of defence mechanism to let you rest the injured area and let healing process to take place
During inflammation process the brain has received information of the injury and extra blood flows to the injured area and this let white blood cells to form a clot to stop the body from loosing more blood and start the healing process
 
Duh sasa tungeomba tafsili na sisi wengine tujue tukateke vijiwe kariakoo
 

Umetisha. Hapo kwenye red ndicho kitu ambacho nilikuwa nakikosa kwenye mawazo yangu. Asante sana. Ila naomba kuuliza zaidi.
(1) Kama maumivu ni sehemu ya mwili kijilinda halafu mimi nikatumia dawa ya maumivu na kuendelea na mambo yangu si nitakuwa najiumiza sasa?
(2) Sababu uliyoitaja hapo juu ni sawa na kwenye sababu ya kuvimba mtoki? Asante.
 
Upo vyema
 
Kwa ufupi uvimbe ni mfumo wa mwili kujilinda dhidi ya mashambulio ya vimelea. Ipo hivi, mwili unaposhambuliwa tuseme na bakteria kama streptococcus taarifa inapokelewa haraka na antibody ambazo ndio askari walinzi wa mwili na muda wote wapo doria. Hawa huja haraka na wakisaidiwa na vikosi toka kwenye lymph nodes mfano T cells na B cells. Hawa wanatengeneza kitu kinaitwa karantini yaani inawakusanya pamoja vimelea na kuwazunguka. Hapa uvime utatokea na katika uvimbe zile cells za msaada huwashambulia hao vimelea. Mfano wa askari hao toka chembe hai nyeupe ni killer cells, suppresor, memory n.k. Pia lysosome na phagocytes huwa sambamba katika kuua na kumeng'enya vimelea. Katika kipindi cha mpambano huu, vimelea nao hujaribu kujitetea. Mpambano huu hupelekea mahali palipovimba kuwa na joto/pamoto. Vimelea vikifa na kuondolewa kama taka uvimbe huondoka.

Vimbe kama zile zitokeazo baada ya kujigonga au kupigwa mechanism ni hiyo hiyo. Ukijigonga cells hufa na kupelekea antibody kuzichukulia cells mfu kama antigen/maadui na mpambano huwa kama nilivyoelezea juu.

Jumong S
 
Imebidi kwanza nipite kwenye profile yako nilichokiona na comment uliyotoa mamdogo hukujiunga bahati mbaya jamii forum heshima yako
 
Anti pain zinatumika kama kutia ganzi tuu sehemu yenye maumivu na siyo kujiumiza
 
Asante mkuu. Nadhani umejibu pia swali langu la pili la nyongeza hapo juu. Naomba sasa niweke "rekodi" zangu vizuri, Nitakuwa sahihi nikisema kuwa kila wakati nikiona mtoki maana yake kuna bacteria walishapenya kupitia sehemu iliyo wazi kama kidonda?
 
Anti pain zinatumika kama kutia ganzi tuu sehemu yenye maumivu na siyo kujiumiza
Kujiumiza ninakozungumzia ni kama vile nimeshatumia dawa ya maumivu na nimekuwa na ganzi hivyo nitaendelea kuukanyagia mguu uliokuwa unauma wakati mwili ulishatengeneza maumivu ili niupumzishe.(sijui kama umenielewa?)
 
Yah mumivu ni kukufanya usihangaike ili kizidisha uharibifu uliokwishatokea dawa za maumivu zinapumbaza cell zinazopeleka ujumbe wa maumivu kwenye ubongo na kukufanya uendelee na shughuli zako kama kawaida lakini maumivu yakija na homa na joto la mwili ni dalili ya maambukizi.
 
Asante mkuu. Nadhani umejibu pia swali langu la pili la nyongeza hapo juu. Naomba sasa niweke "rekodi" zangu vizuri, Nitakuwa sahihi nikisema kuwa kila wakati nikiona mtoki maana yake kuna bacteria walishapenya kupitia sehemu iliyo wazi kama kidonda?
Mwili unafanya kazi kama kitu kimoja, kidonda kikiwa mguuni cells zinaungana na musclesa kupokea maumivu na wewe kusikia maumivu ya mtoki ni ishara ya kuwa mguu hauko katika hali nzuri
 
Kujiumiza ninakozungumzia ni kama vile nimeshatumia dawa ya maumivu na nimekuwa na ganzi hivyo nitaendelea kuukanyagia mguu uliokuwa unauma wakati mwili ulishatengeneza maumivu ili niupumzishe.(sijui kama umenielewa?)
[emoji4] [emoji4] sizani kama utaweza kuwaza kuukanyagia mguu ulio vunjika au kuchoma na msumali kisa umepata dawa za kutuliza maumivu
Hapo hata uwoga ni tiba
 
Asante mkuu. Nadhani umejibu pia swali langu la pili la nyongeza hapo juu. Naomba sasa niweke "rekodi" zangu vizuri, Nitakuwa sahihi nikisema kuwa kila wakati nikiona mtoki maana yake kuna bacteria walishapenya kupitia sehemu iliyo wazi kama kidonda?
Mtoki ni too wide mkuu. Mtoki au swollen lymp nodes/glands ni moja kati ya mifumo ya ulinzi. Ipo standby in some areas za mwilini mfano nyongani, shingoni, na kwapani. Key reasons za mtoki ni kuwa na mashambulizi ya vijidudu au kuumia. Kazi kuu ya mtoki ni kugundua maambukizi. Magonjwa mengi hupelekea mtoki, mf UKIMWI, kansa, joint diseases n.k.

Uvimbe wa mtoki ukizidi kuwa mkubwa seek medical advice hosp.
 
ASANTE
 
Thanx
Na umevitendea haki vidole vyako kwa maelezo haya uliyotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…