Wizara ya Ardhi
Member
- May 14, 2024
- 94
- 75
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amefanya kikao kazi na wataalamu wa Idara ya Maendeleo ya Makazi pamoja na Idara ya Upimaji na Ramani Agosti 13, 2024 ambacho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara Mtumba jijini Dodoma.
Soma Pia:
Katika kikao hicho Ndejembi amewataka wataalamu wa idara hizo kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo ya taaluma zao hatua inayowasaidia kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya wizara ili kuwahudumia Watanzania.