Wataalamu wa Currency naomba mnisaidie.

Wataalamu wa Currency naomba mnisaidie.

queenkami

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2010
Posts
1,694
Reaction score
1,249
Habari zenu wakuu.

Wakuu naomba kueleweshwa,
kwanini mtu ukienda sehemu wanazobadilisha pesa hapa Tanzania ukiwa na noti moja ya dola mia na ukiwa na dola mia ambayo iko kwenye noti nyingi nyingi za say dola moja moja,dola kumi au hamsini thamani yake ni ndogo kuliko ile ya dola mia iliyoko kwenye noti moja na dola mia.

Nauliza hivi kwa sababu nimeshakutana na hii kitu mara nyingi ninapobadilisha pesa,je nimekua na bahati mbaya ya kukutana na matapeli au ndivyo ilivyo?

Pili,kwanini mtu ukiwa na noti ya shilingi(madafu)iliyochanika kidogo unaweza kununua nayo kitu lakini ukiwa na noti ya dola iliyochanika kidogo wanakubali kuibadilisha lakini kwa thamani ndogo sababu imechanika.Sielewi kwanini ishuke thamani ikiwa wanaipokea.

Asanteni.
 
Kuhusiana na hela kuchanika nafahamu ni either kwenye bank of tanzania act au bankng and financial institutions act ya tanzania ni kwamba hela ikiwa damaged in either way benki inaweza kuikataa au ikakupa ya chini yaa thamani yake labda na hao watu wanafuata trend hiyo..kuhusiana na dola dola 1 moja nadhani wanaona haina faida kwaio ni jukumu lako kuikataa pindi mtu anapotaka kukupa note yake maana wengi wanai equate na 1000tshs
 
dola ndogo ndogo hazina thamani nchini kwetu kwavile haziko kwenye mzunguko wa matumizi kama ilivyo shillingi, so maduka ya fedha yanaponunua toka kwako ni kama wanakaa nazo tu, hazitoki kivile, so in a way ni kama wana-discourage wateja wasilete, ni business strategy tu
 
Back
Top Bottom