Pre GE2025 Wataalamu wa Haki za Binadamu wa UN watoa wito kwa Tanzania kumaliza ukiukwaji wa haki za binadamu kuelekea chaguzi za 2024/2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
GENEVA (17 Oktoba 2024) – Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa Tanzania kumaliza ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia, waandishi wa habari, na watetezi wa haki za binadamu.

Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2024 na uchaguzi wa Rais Oktoba 2025, matukio ya kukamatwa kiholela, utesaji, mauaji haramu, na kizuizi cha uhuru wa kujieleza yameongezeka.

Pia, wataalaamu hao wameelezea wasiwasi juu ya kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari na kuwekewa vizuizi mitandao ya kijamii, na wamesisitiza serikali irejeshe upatikanaji wake mara moja.

Pia wamesifu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Arusha wa kusimamisha kwa muda uamuzi wa serikali wa kufuta na kuondoa vijiji katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kutoka orodha ya wapiga kura, na wamehimiza mazungumzo zaidi na watu wa Maasai kutafuta suluhisho endelevu linaloheshimu haki zao.

==========================​

"Tanzania: Experts call for urgent action amid crackdown on civil society ahead of elections | OHCHR" https://www.ohchr.org/en/press-rele...ent-action-amid-crackdown-civil-society-ahead
 
Hii lugha mama angu haijui. Mtafsirie basi.

Atasema hajasikia
 
Yule jamaa wa DSM alonyanyua tofali/jiwe na kumtwanga mwenzie mchana kweupee ingekuwa usiku .....
Ivi alopigi anaendeleaje
Siasa zinatuvuruga na kutufanya watumwa
 
Chadema na vyama vyengine vimekosa mwelekeo. Badala ya kuwekeza kwenye kuwashawishi wapiga kura wamebaki kulalamika na kutaka huruma ya wazungu.

Wana CCM wanahimizana kujiandikisha. Wapinzani wao wanafurahia watu kutojiandikisha alafu matokeo yakitoka wanaanza kutukana Walimu na Polisi
 
madai mafao bana 🤣
 
Drones za Israel kwann haziji hapa Tanzania kuwanyakuwa hawa viongozi viziwi??
 
UN Human rights experts ni chadema? Nafikiri wewe hujui siasa kadri CCM wanavyohimiza wananchi kujiandikisha ndivyo wanavyojichimbia kaburi lao.
 
Una akili fupi sana wewe,unafikiri bila mataifa ya ulaya kuingilia kati,ccm itatoka madarakani??katiba mpya tu hawaitaki,tume huru ya uchaguzi imewashinda
 
msitupangie sisi ni nchi huru mkome kabisa
 
Wamefika Gaza, Lebanon, CongoDr ambako Marekani anafadhili operation chinjachinja, mtoto wa miaka miwili anatupiwa bomu la kilo 800?
 
wapinzani ni wahuni kuliko uhuni wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…