Kuna mtaalamu mmoja anatrend kwenye mitandao akihojiwa na kituo kimoja cha radio na kusema wanaoandika majibu ya malaria kwa mtindo huo ni waongo huku akienda mbali zaidi na kusema waripotiwe haraka kwa mamlaka ili wachukuliwe hatua.
Mimi binafsi namuona huyu mtu ni mhuni na sidhani kama ana weledi.
Sababu za kusema hivi ni kwamba,hao wataalamu wanaoandika hivi,wapo nchi nzima hadi vituo vya serikali.Wameandika hivyo kwa miaka mingi na hakuna mtaalamu yeyote alikemea.
Madaktari wanapokea majibu na kuandikia wagonjwa dawa.
Katika hospitali za serikali,hata ripoti za saa 24 utakuta wanatambua majibu kama hayo ya plus plus.
Leo inawezekanaje mtu mmoja kashiba maharage anakuja kusema huo ni uongo?
Ningemwelewa sana iwapo angesema katika miongozo mipya,wamependekeza kubadili namna ya kuripoti ungonjwa wa malaria,ningemwelewa.Lakini kusema waliokuwa wanaandika +++ ni uongo,ama waliokuwa wanaandika 3 rings ni uongo,mimi sitamwelewa kabisa.Namuona ni mmoja wa vijana wa hovyo wanaosoma siku hizi na wanadhani watu wote waliosoma zamani ni wapumbavu! Maana haiingii akilini wataalamu nchi nzima wawe na mtindo mmoja wa kuandika bila kufundishwa vyuoni.
Vyuo vingi vinavyofundisha wataalamu wa maabara ni vya serikali.Kwa hiyo ni sawa na kutaka kutwaambia walifundishwa matango pori.Vinginevyo alipaswa kutwambia ni mfumo mpya tu wa kuripoti umebadilika na sio kutuambia walivyoandika ni uongo.
Na kama kweli walivyokuwa wakiandika ni uongo,basi mfumo mzima wa afya ni wa kitapeli.Maana madaktari hawajawahi kutuambia hili ijapokuwa majibu haya huwa tunayapeleka kwao na wanatuandikia dawa.Yaani nchi nzima wataalamu wa afya walikuwa vilaza ila kaja huyu jamaa ndiye mtaalamu tena wa WHO!
Kwa jinsi hii,nitaamini kweli nchi hii mapapai yana korona,gono,kaswende na UTI
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app