Wataalamu wa magari mtufahamishe juu ya uchinjaji wa magari

Wataalamu wa magari mtufahamishe juu ya uchinjaji wa magari

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Kila nipitapo hapa temeke mwisho asubuhi nakutana na pilika pilika za uchinjaji wa haya magari, kinacho nishangaza jinsi ya magari muonekano wake wa nje unaona kabisa body imenyooka haina shida.

Leo nimekuta TATA MBILI NAMBA D wanazichinja nikabaki nastajabu na kujiuliza maswali mengi,shida inakuwa wapi mpaka haya magari kuchinjwa? Nikiziangalia kwa nje mpaka seat zake zinavutia. Nikajiuliza tena au zimekufa ENGINE?

Basi wenye kujua/uelewa wa uchinjwaji wa haya magari naomba watupe elimu kidogo ili tukipita basi tuone hali ya kawaida tusiwe na maswali lukuki kichwani.

NB: KUOA NI SAWA KUCHUKUA KITU KIZANI NA KUKILETA KWENYE MWANGA.
 
Magari ya Bima hayo..ukichinja unapata pesa mingi kuliko kuuza zima..mfano unanunua Gari ya Bima lililopata ajali milioni tatu ukichinja hukosi milioni nane
oooh, lakini haya hayana ajari hata mchubuko ninayoonaga mimi

shukrani
 
oooh, lakini haya hayana ajari hata mchubuko ninayoonaga mimi

shukrani

Unaweza ukapata gari kwa bei nzuri zima, ukalichinja likakupa faida mara mbili, kuliko kutafuta mteja na kubagain upyya bei ya gari zima.
 
kuchinjwa kwa magari ndio kufanyaje??
Kupangalua gari nzima na kuanza kuuza kifaa kimoja kimoja, i.e. engine inauzwa kivyake, milango kivyake, vioo kivyake, bodi kivyake mpaka mzigo mzima unaisha. Biashara za Temeke na Tandale hizi
 
Kupangalua gari nzima na kuanza kuuza kifaa kimoja kimoja, i.e. engine inauzwa kivyake, milango kivyake, vioo kivyake, bodi kivyake mpaka mzigo mzima unaisha. Biashara za Temeke na Tandale hizi
asante kwa ufafanuzi zaidi kuna mtu kishanielekeza maana ake pia
 
Nami nikitaka kuchinja langu nafanyaje aisee, kuna madalali naongea nao wanashughulikia au inakuwaje wakuu kwa mwenye uelewa hapo.
 
Nami nikitaka kuchinja langu nafanyaje aisee, kuna madalali naongea nao wanashughulikia au inakuwaje wakuu kwa mwenye uelewa hapo.
gar yako n aina gan na iko wapi....hakikisha una kadi ya hyo gari
 
Nami nikitaka kuchinja langu nafanyaje aisee, kuna madalali naongea nao wanashughulikia au inakuwaje wakuu kwa mwenye uelewa hapo.

Unaweza kutumia madalali as well as wauzaji wa spare/mazagazaga used ambao wako exposed na soko!
 
Back
Top Bottom