Wataalamu wa mambo haya

Wataalamu wa mambo haya

kizoleo

Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
79
Reaction score
8
Wakuu ni muda gani huchukua baada ya mwanamke kutoka kujifungua, na kuanza mzunguko wa siku zake?
 
hapa mimi empty kabisaa, sitaki kuku-mislead.....watakuja wenyewe wenye kazi zao.....:wave:
 
Wakuu ni muda gani huchukua baada ya mwanamke kutoka kujifungua, na kuanza mzunguko wa siku zake?
kama atamnyonyesha mtoto kama inavyotakiwa,bila kumpa mtoto kitu kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama tuu(exclusive breastfeeding) basi hatapata hedhi kwa kipindi chote hicho atakavyofanya hivyo(kitaalam,mama anatakiwa amnyonyeshe mtoto maziwa yake tuu kwa muda wa miezi 6 ndipo aanze kuongeza na vitu vingine)
 
Ahsante kwa majibu mazuri dr. Je kwa mtu kama huyu ana nafasi gani katika kushiriki tendo la ndoa bila kupata mimba zisizo tarajiwa ukilinganisha na muda atakaokaa bila kuona mzunguko wa siku zake?
 
Wakuu ni muda gani huchukua baada ya mwanamke kutoka kujifungua, na kuanza mzunguko wa siku zake?
Mkuu hakuna jibu la pamoja kwa swali lako kwa sababu kila mwanamke ana hormone tofauti na mwingine,ila wanawake wengi hupata siku zao baada ya wiki 10,baadhi ya wanawake wanaponyonyesha watoto wao huwa hawapati siku zao hata zaidi ya mwaka,kwa wale wanaonyonyesha watoto wao bila kuwapa vyakula vingine huchelewa zaidi kupata siku zao kuanzia wiki 20 na kuendelea kuliko wale wanaowahi kuwapa vyakula vingine mbali na maziwa ya mama.
 
Back
Top Bottom