Wataalamu wa matangazo ya biashara/marketing hebu nielimisheni

Wataalamu wa matangazo ya biashara/marketing hebu nielimisheni

Lukansola

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
5,435
Reaction score
1,604
Habari zenu wakuu, nitaongea kwa kifupi tu:
Kero yangu ni haya matangazo ya biashara ya kibongo, leo nizungumzie tangazo la Airtel Money ambalo yupo Majuto na sharobaro mmoja ambaye simjui, juzi tena nikiangalia TV nikaona watu hao hao wawili tena wakiwa almost in same outfit, (kwa mfano yule sharobaro alikuwa na mi-plaster usoni kama) wakiwa wanatangaza sijui sayona sijui sippy soda... (hata sikumbuki).

Sasa mimi nilifikiri tangazo la biashara linapaswa kuwa unique kwa kila kitu ili liweze ku maintain identity ya tangazo husika, yani kama ni sauti za watu kwa mfano, hazitakiwi tena zisikike kwenye ku promote product nyingine au costume inapaswa kuwa ya namna tofauti na matangazo ya bidhaa za makampuni mengine. au nakosea?

Halafu ni nani aliwaambia matangazo ya biashara ni lazima yawe comic? kwani bila kuchekesha vichekesho ambavyo havichekeshi hamuwezi kutengeneza tangazo likauza? kwa hiyo tutegemee kumuona huyo majuto kwenye matangazo ya kila bidhaa ya tanzania kuanzia magodoro, masufuria, vikombe nk?

Nawasilisha hoja wakuu.
 
Hata mimi matangazo yao hunikera sana hasa wanapomaliza kwa kuchezacheza ngoma. Yaani ubunifu ni zero.
 
ronaldinyo alivunjiwa mkataba wa £72,000/= na pepsi kwa kunywa kola
 
Hata mimi matangazo yao hunikera sana hasa wanapomaliza kwa kuchezacheza ngoma. Yaani ubunifu ni zero.

Sasa sijui ngoma na mpiga debe wapi na wapi, umenikumubsha tangazo lingine la magodoro nalo uozo tu...

pia kuna tangazo lingine la magodoro yupo Bambo, basi lile tangazo ni matusi matupu (kwa mtazamo wangu) pale mwisho jamaa anasema kukuruka mwanangu halafu anafanya kama mtu anyefanya mchezo mmbaya vile, huwa nawashangaa sana wanaotengeza haya matangazo na wale wanaoya-approve yatoke, ni vichekesho kwa kweli.
 
Back
Top Bottom