Cha muhimu hapo mkuu ni uwekeze kwenye drawing tablet nzuri, cha pili ni ujue kustudy hizi art/illustration.
Kwanza, picha kama hii imechorwa kwa kutumia reference photo, pia halisi inakuwa imported kwenye artboard then mchoraji anakuwa anatrace sketch kwa kutumia drawing tablet. Ni muhimu kuwa na drawing tablet kwa sababu itasaidia kuchora details halisi hasa kwenye nywele.
Pili, baada ya sketch yako unaweza kusample rangi zote zilizopo kwenye picha halisi na ukazitenga pembeni(hii ni kwa beginners) . Rangi zote kuanzia nywele, lips, ngozi, highlights na shadows (ingawa shadows ni rangi ya ngozi iliyofifia kidogo.)
Tatu, unaanza kuapply rangi kwenye sehemu husika, utaanza na ngozi, na sehemu muhimu, then utafuata kwenye shadows na mwisho kabisa ni highlights.
NB: Maelezo haya ni kwa mtu asiyejua kuchora kabisa. Unahitaji kuwa na subira maana wakati unaanza kuchora hutaweza kunotice mabadiliko lakini art ikishamalizika ndiyo utagundua umeenda kiasi gani.
Mcheck jamaa youtube anaitwa ChiWorld1234 anatutorials ambazo zitakuwa walkthrough ya uchoraji wa digital art mwanzo mpaka mwisho.
Hii ni moja ya kazi za Chiworld1234
View attachment 2236884