Wataalamu wa Sayansi tujuzeni hili

Wataalamu wa Sayansi tujuzeni hili

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Kuna radi kali sana imemulika hapa mjini Morogoro muda huu, ikafuatiwa na mlio mkali wenye kushitua kama bomu, sauti hiyo kali imetikisa madirisha makabati nk.

Swali:
Mawimbi ya sauti yanawezaje kusababisha vibrations kali kiasi hicho cha vioo kujibamiza?
 
Hiyo radi na mimi nimeiona na kuskia muungurumo wake,ni shida mpaka watoto wameangua vilio hapa
 
Pole mkuu, kulikuwa na wataalamu wa radi humu sijui waliishia wapi, may be hawajaamka
Hili sio utaalamu wa radi ni sauti.

Mweka mada usishangae sauti inaweza kufanya vitu vitikisike ndio maana sauti husafiri kwenye hewa(molecules).

Najikuta nakosa maelezo anyway wenye lugha rahisi watakujibu kiundani
 
Ki science inawezekana ila kitamaduni haiwezikani. Lakini yawezeka radi ili strike hapo
 
Huo mwanga unaouona ndio radi yenyewe, ambayo ndio inaweza kuleta madhara Kwa kitu chochote kinachoingilia njia yake

Huo muungurumo Hauna madhara yoyote ingawa unaweza kuwa mkali mpaka kusababisha mtikisiko wa baadhi ya vitu
 
Mawimbi ya sauti yanawezaje kusababisha vibrations kali kiasi hicho cha vioo kujibamiza?
sound waves yanasafiri kwa ku push air molecules, ambazo ni maada pia,
chukulia 'air molecule' kama 'jiwe' vile, japo halionekani, ila lina impact liki gain speed kuleta shock wave

mawazo yangu hayo
 
Kuna radi kali sana imemulika hapa mjini Morogoro muda huu, ikafuatiwa na mlio mkali wenye kushitua kama bomu, sauti hiyo kali imetikisa madirisha makabati nk.

Swali:
Mawimbi ya sauti yanawezaje kusababisha vibrations kali kiasi hicho cha vioo kujibamiza?
Hiyo sauti uliyoisikia siyo radi yenyewe, ni matokeo ya radi. Chaji hasi na chanya zimekutana na kugongana, na baada ya hapo ndiyo sauti ikatokea. Chaji zilizogongana zimesababisha uwepo wa mechanical energy, pamoja na sound energy. Kwa hiyo kilichosababisha mtikisiko ni ule mgongano wa chaji hasi na chanya na siyo mwanga au sauti uliyoisikia
 
Huo mwanga unaouona ndio radi yenyewe, ambayo ndio inaweza kuleta madhara Kwa kitu chochote kinachoingilia njia yake
Asante Mkuu, je kuna namna ya kujua njia yake ili kuepuka kuiingilia kama vile tunavyofanya kwa train?
 
Chaji zilizogongana zimesababisha uwepo wa mechanical energy, pamoja na sound energy. Kwa hiyo kilichosababisha mtikisiko ni ule mgongano wa chaji hasi na chanya na siyo mwanga au sauti uliyoisikia
Hapa ndipo natamani sana kupaelewa kwakuwa nime relate na siku moja walipita CUF na maspika makubwa wanafanya kampeni, sisi tulikuwa kama mita 80 toka barabarani na tulikuwa kwenye gari lakini tulisikia mtikisiko kutokana na sauti zile kali na kishindo cha muziki
 
sound waves yanasafiri kwa ku push air molecules, ambazo ni maada pia,
chukulia 'air molecule' kama 'jiwe' vile, japo halionekani, ila lina impact liki gain speed kuleta shock wave

mawazo yangu hayo
Asante Mkuu naanza kupata idea
 
Hapa ndipo natamani sana kupaelewa kwakuwa nime relate na siku moja walipita CUF na maspika makubwa wanafanya kampeni, sisi tulikuwa kama mita 80 toka barabarani na tulikuwa kwenye gari lakini tulisikia mtikisiko kutokana na sauti zile kali na kishindo cha muziki
Nadhani kinachotokea hapa ni conversion tu ya energy from sound to Mechanical energy. Kumbuka kuwa energy can be converted from one form into another. Anayefahamu zaidi kuhusu namna spika zinavyofanya kazi anaweza kusaidia zaidi katika hili.
 
Asante sana Mkuu
 
Back
Top Bottom