Wataalamu wa sheria pitieni hapa

Wataalamu wa sheria pitieni hapa

Joined
May 19, 2023
Posts
20
Reaction score
34
Naomba kujua kama mtu aliomba mkopo then katika mkataba yule mtoa mkopo hakuweka kipengele cha "madhumuni ya mkopo",je ikitokea shida mbele ya safari yupi anafaidika mkienda mahakamani?
 
Wanasheria na Majaji wanakuja Mkuu.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mkuu lipa deni la watu usitafute excuse

Kisheria unapaswa kulipa deni kulingana na mkataba

Habari ya madhumuni ya mkopo ingekuwa muhimu ingewekwa kwenye masharti ya mkopo wenu
 
Kwamba kwa kuwa hajaweka dhumuni la mkopo ndicho kigezo cha kukwepa deni?

Labda ungeniambia kwamba mkopeshaji hana uwezo wa kisheria wa kukukopesha.

Lipa deni la watu haloo!

Kwani ulikopa benki, kikoba, mtu binafsi, chupi mkononi au kausha damu?
 
Kama haujaelewa ni heri kukaa kimya kuliko kuleta ujuaji usio na faida na mwisho ni kuonekana mweupe kick kichwani,
 
Uwezo wako w kufikili ndo ulipoishia,km haujui sheria n heri ukae kimya,si lazima u uchangie kila kitu?
 
Naomba kujua kama mtu aliomba mkopo then katika mkataba yule mtoa mkopo hakuweka kipengele cha "madhumuni ya mkopo",je ikitokea shida mbele ya safari yupi anafaidika mkienda mahakamani?
Inategemea shida inatokea kwenye suala gani? mfano;
1: Mkopo kutumika kwa shughuli ambazo hazikuwa katika mkataba?
2: Ucheleweshaji wa marejesho?
3: Kutokulipwa kwa mkopo?

Nafikiri kupitia baadhi mifano hapo juu ndio inaweza kutoa mwanga wa namna bora ya kutoa ushauri katika tatizo lako
 
Mm ndo niliomba mkopo lkn sikupewa mkopo huo,hadi bank wakaanza kunikata kwenye mkopo bila kuwa wamenipa mkopo,sasa nilikuwa napatiwa ushauri na mdau ndo akaniuliza kuhusu kipengere cha dhumuni la mkopo ili anisaidie namna ya kudai fidia,mm nikamjibu kuwa ktk mkataba ule sikuona kipengere cha dhumuni la mkopo,,,ndo maana nikaona nitafte msaada pengine kwa ufafanuzi na si vinginevyo
 
Kwamba kwa kuwa hajaweka dhumuni la mkopo ndicho kigezo cha kukwepa deni?

Labda ungeniambia kwamba mkopeshaji hana uwezo wa kisheria wa kukukopesha.

Lipa deni la watu haloo!

Kwani ulikopa benki, kikoba, mtu binafsi, chupi mkononi au kausha damu?

Nini mkononi tena au umekosea?
 
Mm ndo niliomba mkopo lkn sikupewa mkopo huo,hadi bank wakaanza kunikata kwenye mkopo bila kuwa wamenipa mkopo,sasa nilikuwa napatiwa ushauri na mdau ndo akaniuliza kuhusu kipengere cha dhumuni la mkopo ili anisaidie namna ya kudai fidia,mm nikamjibu kuwa ktk mkataba ule sikuona kipengere cha dhumuni la mkopo,,,ndo maana nikaona nitafte msaada pengine kwa ufafanuzi na si vinginevyo
kwa maelezo yako hapa, unachodai wewe ni kukatwa pesa kwa ajili ya marejesho ya mkopo ambao hujapata"huwezi lipa ambacho hujapokea".
yuko sahihi kukuuliza dhumuni la mkopo,kwani inawezekana kiasi hicho cha mkopo kuwa kimeshaelekezwa katika kitu husika mfano; uliomba mkopo kwa ajili ya ada ya mtoto wa chuo,hivyo unaweza kuta moja kwa moja umeshaelekezwa sehemu husika,licha ya kuwa ulipaswa kupata taarifa kuwa mkopo ulioomba tayari umeshatoka na umeelekezwa mahali husika.
Nafikiri ulipewa nakala(copy)ya mkataba wa mkopo jitahidi kumpatia ausome sababu lazima kipengele cha dhumuni la mkopo kiliwekwa ,japo inaweza kuwa hakuonyesha moja kwa moja kuwa ni DHUMUNI LA MKOPO ila ulikuwepo katika mkataba ,hivyo jitahidi kumpa mwanasheria au mshauri wako wa sheria huo mkataba ili aupitie ndipo taratibu zingine zifuate kama kuandika Demand Letter kwa benki husika.
 
Naomba kujua kama mtu aliomba mkopo then katika mkataba yule mtoa mkopo hakuweka kipengele cha "madhumuni ya mkopo",je ikitokea shida mbele ya safari yupi anafaidika mkienda mahakamani?
Dhumuni la Mkopo analijua Mkopaji,hata kama atakwenda olea mke wa pili, hilo halimuhusu mkopeshaji! Lipa deni achaa visingizio!! Hii imeenda!!
 
Duh,lakini kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na malalamiko mingi Sana katika Taasisi hizi za kifedha(Benki) katika mikopo,nafikiri pia ni wakati was mkopaji na mkopeshaji kujitathimini kwanza

Tatizo la mbongo ana sign mkataba wa mkopo kabla hajausoma,na Bank walivyo wahuni wanakwita siku hiyo hiyo wanakupa mkataba usaini hapo hapo wakati wanajua kabisa huo muda ni mdogo sana na huwezi pitia krassa zote ,zaidi utaangalia mshiko umewekewa ngapi na kwa mwezi wanakata ngapi,basi wwe faster unaanguka sign yako! Sasa yakitokea ya kutokea huko mbele,bank wanakuambia rejea mkataba wako kwanza alafu ndiyo uje tena!!!
 
Kama haujaelewa ni heri kukaa kimya kuliko kuleta ujuaji usio na faida na mwisho ni kuonekana mweupe kick kichwani,

Ukweli unauma..... usitafute janja ya kukwepa kulipa deni mkuu

Ungeuliza kuhusu riba kubwa au uonevu fulani ungeeleweka

Swali lako japo umeli edit lakini lina mlengo wa kupokea hela za mkopo halafu huko mbeleni utafute sababu ya kutokulipa HUU NI WIZI

Kanuni ya msingi ni moja tu ...... LIPA DENI usitafute excuses
Huwezi basi usichukue mkopo wa watu
 
Naomba kujua kama mtu aliomba mkopo then katika mkataba yule mtoa mkopo hakuweka kipengele cha "madhumuni ya mkopo",je ikitokea shida mbele ya safari yupi anafaidika mkienda mahakamani?
Malengo ya mkopo siyo kigezo sana, kikubwa ulikopa hivyo rudisha. Hata kama ulitumia kunywa gongo hiyo ni juu yako.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom