Wataalamu wa sheria za soka hebu tutoeni tongotongo kuhusiana na BUYOUT CLAUSE na RELEASE CLAUSE,maana tunachanganywa mno

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Kuna mwandishi mmoja ameelezea suala la saga la Faisal hivi.....

Feisal Salum kama katekeleza kipengele cha kununua mkataba wake hilo halina shaka linawezekana duniani kote, lakini inasalia Azam FC kumalizana na Yanga kulingana na VALUE ambayo Yanga watampa Mchezaji wao, vipi kama Yanga wakisema thamani yake ni BILLION MOJA? Itapaswa kulipwa ili ajiunge na Azam.

Kipengele kilichosalia ni Yanga Vs Azam, haitokuwa vita rahisi ndani ni SHERIA na PESA, tunasubiri kuona drama inaishaje ila hii kitu kwenye meza ya sheria na kanuni za FIFA bado haijaisha ni mbichi mno kama kweli Feisal kanunua mkataba.

Ulaya wengi wanachofanyana ni kumalizana na klabu kisha Mchezaji ili wasikomoane.

Kuna vitu viwili RELEASE CLAUSE na BUYOUT CLAUSE, sidhani kama Yanga wanaweza kuwa wajinga kiasi hicho waachie room ya Feisal kuondoka kirahisi[emoji3]! Kama vyote vipo maana yake Azam wanapaswa kurudi Jangwani kumalizana na Yanga endapo waliweka vyote viwili.

Najaribu kuwaza hii room ya kisheria maana ni ajabu mno Mchezaji kama Feisal kupatikana kirahisi hivyo, nje na hapo basi Yanga watakuwa wamefeli kwenye eneo la Kitengo cha sheria kama itaenda tofauti.

Ila nilichokuwa nafikiri mtu akinunua mkataba wake anakuwa yupo huru,mfano faisal akinunua huo mkataba anaweza kujiamulia kukaa nyumbani akafanya mambo yake,au mimi ndio sielewi?
Msaada please[emoji120]
 
Kumbe na wewe huelewi?
Hata sisi hatuelewi
 
Mwingine anasema hivi


KUHUSU FEISAL SALUM ABDALLAH

Kwanza ni KWELI pasi na shaka yoyote kwamba Feitoto amewapa NOTISI klabu yake ya Yanga SC ya kuvunja mkataba nao.

Feisal alikuwa na mkataba na Yanga SC (ambao BIN KAZUMARI imeuona) uliosainiwa tarehe 10 Agosti 2020 ukichukua nafasi ya ule uliosainiwa 2018. Mkataba huu unamalizika tarehe 30 Mei 2024.

Kipengele cha 2.3 cha mkataba kinazungumzia pesa ya usajili ambayo ni Tshs 100,000,000/= kwa kipindi chote cha mkataba ambacho kimsingi ni miaka 4 (2020 - 2024).

Kama ilivyo mikataba mingi kwenye mkataba huu pia kuna vipengele vya KUVUNJA mkataba ambacho ni namba 14 (Expiry, suspension and termination of the contract).

Katika kipengele namba 14.7 kama kilivyonakiriwa kwenye barua (notisi) ya kuvunja mkataba (swipe left) kinampa haki mchezaji kuvunja mkataba katika hali isio ya kawaida kwa kulipa pesa ya usajili kama inavyoainishwa na kipengele cha 2.3 na walau mshahara wa miezi 3.

Ukisoma katika kipengele cha 5 kinachozungumzia mshara, bima na malipo/ada nyingine (salary, insurance and other fees ) utagundua kipengele cha 5.1 kinasema mshahara wake ni Tshs 4,000,000/= kwa mwezi. Kwa miezi 3 kama unataka kulipa manake ni Tshs 12,000,000/=

Hiyo ndiyo sababu ukisoma notisi ya kuvunja mkataba inasomeka kwamba Feisal AMEILIPA Yanga SC Tshs 112,000,000/= ili kuendana na takwa la kimkataba. Kwamba milioni 100 pesa ya usajili na milioni 12 mshahara miezi 3.

Kipengele cha 18 ambacho ni cha mwisho kabisa katika mkataba kinazungumzia UHAMISHO WA BAADAE (Future Transfers). Ambapo 18.1 imasema "Mchezaji anaweza kuhamishwa kwenda klabu nyingine kukiwa na haja hiyo. Klabu inaweza kuanzisha mazungumzo na kufanya jitihada zake zote kuhakikisha usajili huo unafanikiwa juu ya kwamba klabu itaweka na kuamua pesa ya uhamisho kuendana na soko la wakati huo ambayo haitokuwa chini ya dola za kimarekani laki moja isipokuwa ikiamuliwa vinginevyo na klabu, ada ya uhamisho iliyotajwa itajumuisha mazingatio ya mchezaji kuhamia klabu nyingine"

Baada ya Feisali KUVUNJA mkataba KULIPA na kutoa notisi anakua mchezaji huru anaeweza kujiunga na klabu yoyote kama hakuna kipengele kilichokiukwa. Kipengele cha 18.1 hakiwezi kumbana tena.

BIN KAZUMARI.
 
Chawa yeye amesema hivi....View attachment 2456498
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Sasa huyu Manara ni kama nani? Halipi mshahara wa Feitoto na wala sio Meneja wa mchezaji. Anaongea kama Nani?

Huyu jamaa nimeshagundua ana shida kubwa sana kwenye akili na anahitaji msaada wa kitaalam. Ni talkative sana hata katika ishu ambazo hausiani nazo na pale alipo kafungiwa lakini naona bado anakomaa tu.
 
Kama kilichofanyika ni hiki basi huo mkataba haujavunjwa bali Fei amenunua mkataba wake.
Ko bin kazumari hapa kaingia Chaka.
 
Kama kilichofanyika ni hiki basi huo mkataba haujavunjwa bali Fei amenunua mkataba wake.
Ko bin kazumari hapa kaingia Chaka.
Ndio tunaomba msaada kuhusu hilo,yaani ukinunua mkataba (BUYOUT) Ina maana gani?unakuwa huru au bado unakuwa mali ya klabu na unapaswa kuuzwa?
 
Feisal kanunua mkataba wake na Yanga, yuko huru. Na baada ya kuwa huru akaamua kujiunga na Azam kama mchezaji huru. Hivyo hakuna tatizo lolote la kisheria.

Lakini kiuhalisia kilichofanyika ni hichi.
1. Azam wametoa hiyo pesa kwa Feisal ili aachane na Yanga.

2. Azam wameahidi kumpa mkataba mnoo zaidi (ikiwemo mshahara mkubwa zaidi) ili aachane na Yanga.
 
Ndio tunaomba msaada kuhusu hilo,yaani ukinunua mkataba (BUYOUT) Ina maana gani?unakuwa huru au bado unakuwa mali ya klabu na unapaswa kuuzwa?
Mbona hilo liko wazi sana, mchezaji akivunja mkataba wake kwa kuununua, maana yake anakuwa huru. Na mchezaji akiwa huru maana yake hafungwi tena na chochote kuhusu usajiri wake, popote anaweza kusajiriwa kwa mkataba wowote.
 
Kuna mwandishi mmoja ameelezea suala la saga la Faisal hivi.....

Feisal Salum kama katekeleza kipengele cha kununua mkataba wake hilo halina shaka linawezekana duniani kote, lakini inasalia ...
Yanga haina mwanasheria mwenye uwezo wa kuona mashimo kwenye mkataba. Rejea kesi ya Morrison CAS
 
George Job kapost Instagram kwamba Yanga wameirudisha ile 112M kwenye account ya Feitoto hii ina maana gani? Kulazimisha punda Kunywa maji? Na huko Msimbazi Inonga nae anataka kwenda Azam hataki kusaini mkataba mpya.
 
Ha
Kuna mwandishi mmoja ameelezea suala la saga la Faisal hivi.....

Feisal Salum kama katekeleza kipengele cha kununua mkataba wake hilo halina shaka linawezekana duniani kote, lakini inasalia ...
Hakuna saga yoyote hapo,Faisal ameununua mkataba hiyo ina maanisha kuwa sasa hivi yeye Ni mchezaji huru anaendatimu yoyote anayoitaka,free bila Bei yoyote.
 
Ndio tunaomba msaada kuhusu hilo,yaani ukinunua mkataba (BUYOUT) Ina maana gani?unakuwa huru au bado unakuwa mali ya klabu na unapaswa kuuzwa?
Kuhusu hilo fatilia saga la Neymar na Barcelona, pia fatilia kuuzwa kwa Halaand bei chee kabisa kwenda man city kisha fatilia sakata la coutinho kuondoka liverpool
 
Mfano tukichukulia saga ya Neymar alisaini miaka mitano Barca na kukawa na kipengele kwamba kila dirisha la usajili litakapofika timu itakayoweza kutoa 200m basi ingeweza kumpata Neymar( hapo hakuna kukaa mezani) ilipofika 2017 Neymar akataka kwenda paris, Barca wakakataa mazungumzo, walichofanya paris ni kumpa Neymar hiyo 200m, Neymar alipo iweka tuu kwenye accaunt ya Barca automatic akawa mchezaji huru akajiunga PSG

Kuhusu mkataba wa Fei, yeye na Yanga ndio wanajua ukoje
 
Kuhusu Halaand, aliposain BVB waliweka kipengele kwamba baada ya miaka miwili ikitokea timu itakubaliana na halaand basi ikiwapa BVB 60m anaondoka, ndio maana aliondoka kirahisi bila City na bvb kukaa mezani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…