Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Azam Sio wajinga waingie kichwa Kichwa kuna loophole wameiona wakaingia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamuache aendeGeorge Job kapost Instagram kwamba Yanga wameirudisha ile 112M kwenye account ya Feitoto hii ina maana gani? Kulazimisha punda Kunywa maji? Na huko Msimbazi Inonga nae anataka kwenda Azam hataki kusaini mkataba mpya.
Hahahaaa kwa hiyo tusimwani kabisa. Yaani ni empty kabisaHuyu alikuwepo kipindi kile akagalagazwa na Morrison,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hana cha usomi wala nini
Ahsante,ila naomba kujua kilichofanywa na Faysal si ndio inaitwa BUYOUT CLAUSE????maana kanunua mkataba,kinachochanganya wanasema licha ya hivyo bado inawapasa Azam wawafuate Yanga ili kukubaliana bei ya mchezaji wamnunue hapa ndio sielewi,Kwa ufupi tofauti ya Release clause na buy out clause ni hii;
Release clause inawekwa wakati mnasaini mkataba, inakuwa fixed value, haitabadilika kutokana na muda ambao tayari mchezaji ameshautumikia mkataba au value ya mchezaji kuongezeka au kupungua, release clause itabaki vile vile kama kwenye mkataba, mchezaji muda wowote akiamua kuondoka au timu ikimuhitaji inaweza vunja mkataba kwa kutoa pesa sawa na release clause kwenye mkataba.
- Buy out clause- hii si kuvunja mkataba bali unaununua mkataba wote uliyobakia, mfano mchezaji amesaini mkataba wa miaka 5, ametumikia mkataba kwa mwaka mmoja, una uwezo wa kununua mkataba uliobaki kwa kulipa kiasi chote ambacho alitakiwa kulipwa miaka minne. Hii ni njia ya gharama zaidi hivyo ndio maana timu kujilinda wanaweka release clause kubwa sana ili walazimishe mchezaji akitaka kuondoka ndani ya muda wa mkataba wake, timu pinzani ifanye mazungumzo ya kununua mkataba na sio kutumia “Release clause “.
- Inshu ya Fei Toto, kwa maandishi mbalimbali kwenye mitandoa, Yanga waliweka Release clause ya Fei Toto 100m plus mishahara ya miezi 3, kama Fei Toto amelipa pesa yote ya Release clause hakuna suala la makubaliano mengine hapo ya buy out clause, huo mkataba umeshavunwa na Fei Toto ni mchezaji huru kujiunga na timu yoyote kama atakavyotaka, Yanga wawaambie mashabiki wao ukweli, wasilete siasa kwenye vitu vilivyo wazi.
Hapana, kilichofanywa na Fei Toto ni release clause sio buy out clause, release clause amount yake ipo fixed tayari kwenye mkataba ila buy out clause ndio kuna negotiations. Ni sawa kilochofanywa kwa Halaand kuchukuliwa na Man City kwa ku trigger release clause yake tu toka Dortmund.Ahsante,ila naomba kujua kilichofanywa na Faysal si ndio inaitwa BUYOUT CLAUSE????maana kanunua mkataba,kinachochanganya wanasema licha ya hivyo bado inawapasa Azam wawafuate Yanga ili kukubaliana bei ya mchezaji wamnunue hapa ndio sielewi,
sasa nasikia yanga wamerudisha pesa ambayo fei amewapa
Inonga akienda Azam atatusaidia sana wanasimba siku hizi ana maboko mengiGeorge Job kapost Instagram kwamba Yanga wameirudisha ile 112M kwenye account ya Feitoto hii ina maana gani? Kulazimisha punda Kunywa maji? Na huko Msimbazi Inonga nae anataka kwenda Azam hataki kusaini mkataba mpya.
Ukinunua mkataba una kuwa huru...! Hauendeshwi wala kufungwa na mkataba wa awali maana haupo tena...Ndio tunaomba msaada kuhusu hilo,yaani ukinunua mkataba (BUYOUT) Ina maana gani?unakuwa huru au bado unakuwa mali ya klabu na unapaswa kuuzwa?
Kurudisha haisaidii... hata kwa morrison walifanya hivyo...!George Job kapost Instagram kwamba Yanga wameirudisha ile 112M kwenye account ya Feitoto hii ina maana gani? Kulazimisha punda Kunywa maji? Na huko Msimbazi Inonga nae anataka kwenda Azam hataki kusaini mkataba mpya.
Sisi MSGManara nae anaandika "Fei mkataba wake na sisi"!!!
Mkataba wake mudi aliweka B’ maana aliona timu za tanzania kuna kuzungukana sana...Inonga akienda Azam atatusaidia sana wanasimba siku hizi ana maboko mengi
Ni msomi huyo, ukishakuwa Wakili tayari ni Msomi, haijalishi umeshinda kesi au hujashinda.Huyu alikuwepo kipindi kile akagalagazwa na Morrison,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hana cha usomi wala nini
Huyu wakili kipindi kile alipewa kazi ya kuiwakilisha yanga lakini kosa lilishafanyika kwa yanga yeye Kama wakili ilikuwa kazi yake ni kutetea yanga. Kwa hili la fei kaeleza vizuri kabisa kuwa faeisal anaweza kununua mkataba wake. Hivi kweli yanga unamlipa Aziz k n Morison million za kutosha ala Feisal unamlipa 4mlHuyu alikuwepo kipindi kile akagalagazwa na Morrison,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hana cha usomi wala nini
Sasa Azam wamfuate Yanga ya kazi gani wakati Feisal sio mchezaji wa Yanga tena? Ni mchezaji huru baada ya kununua mkatabaAhsante,ila naomba kujua kilichofanywa na Faysal si ndio inaitwa BUYOUT CLAUSE????maana kanunua mkataba,kinachochanganya wanasema licha ya hivyo bado inawapasa Azam wawafuate Yanga ili kukubaliana bei ya mchezaji wamnunue hapa ndio sielewi,
sasa nasikia yanga wamerudisha pesa ambayo fei amewapa
Mkuu bei ya kununua kitu unajipangia wewe mwenyewe?Sasa Azam wamfuate Yanga ya kazi gani wakati Feisal sio mchezaji wa Yanga tena? Ni mchezaji huru baada ya kununua mkataba
Hiyo 100M na mshahara wa miezi 3 Yanga ndio walioweka mkuu, Feisal yeye katimiza tu matakwaMkuu bei ya kununua kitu unajipangia wewe mwenyewe?
Pia trip na trapKuna mwandishi mmoja ameelezea suala la saga la Faisal hivi.....
Feisal Salum kama katekeleza kipengele cha kununua mkataba wake hilo halina shaka linawezekana duniani kote, lakini inasalia Azam FC kumalizana na Yanga kulingana na VALUE ambayo Yanga watampa Mchezaji wao, vipi kama Yanga wakisema thamani yake ni BILLION MOJA? Itapaswa kulipwa ili ajiunge na Azam.
Kipengele kilichosalia ni Yanga Vs Azam, haitokuwa vita rahisi ndani ni SHERIA na PESA, tunasubiri kuona drama inaishaje ila hii kitu kwenye meza ya sheria na kanuni za FIFA bado haijaisha ni mbichi mno kama kweli Feisal kanunua mkataba.
Ulaya wengi wanachofanyana ni kumalizana na klabu kisha Mchezaji ili wasikomoane.
Kuna vitu viwili RELEASE CLAUSE na BUYOUT CLAUSE, sidhani kama Yanga wanaweza kuwa wajinga kiasi hicho waachie room ya Feisal kuondoka kirahisi[emoji3]! Kama vyote vipo maana yake Azam wanapaswa kurudi Jangwani kumalizana na Yanga endapo waliweka vyote viwili.
Najaribu kuwaza hii room ya kisheria maana ni ajabu mno Mchezaji kama Feisal kupatikana kirahisi hivyo, nje na hapo basi Yanga watakuwa wamefeli kwenye eneo la Kitengo cha sheria kama itaenda tofauti.
Ila nilichokuwa nafikiri mtu akinunua mkataba wake anakuwa yupo huru,mfano faisal akinunua huo mkataba anaweza kujiamulia kukaa nyumbani akafanya mambo yake,au mimi ndio sielewi?
Msaada please[emoji120]
Maelezo yako yanelekea kueleweka lakini unaposema viongozi wa Yanga wanapotosha je ni kiongozi gani umeona kapotosha? Au umeamua kutupa lawama tu?Hapana, kilichofanywa na Fei Toto ni release clause sio buy out clause, release clause amount yake ipo fixed tayari kwenye mkataba ila buy out clause ndio kuna negotiations. Ni sawa kilochofanywa kwa Halaand kuchukuliwa na Man City kwa ku trigger release clause yake tu toka Dortmund.
- Viongozi wa Yanga wanachofanya saivi ni upotoshaji tu ili walinde sura zao mbele ya mashabiki ila hakuna makubaliono yoyote ambayo Azam atahitaji kutoka kwa Yanga kwa sasa.