Wataalamu wasema Askofu Gwajima amepotosha ukweli kuhusu chanjo ya corona

Kama unataka kufanywa panya wa majaribio si nenda tu Kenya, hakukatazi mtu, kila nchi na utaratibu wake

Kila nchi ina utaratibu wake. Utaratibu wa Tanzania uko hapa:



Tupo tunaokataa kufanywa panya wa majaribio na kina Gwajima na pia na mamburula kama nyie.

Kama ya wataalamu hamuyataki si hamtachanjwa mtabakia hivyo hivyo? Shida iko wapi?

Kama la kukaa bila kuchanjwa nalo bado haliwatoshi ila mnaugulia mno kuona wengine tutachanjwa, fikirieni hata kuhamia Burundi.
 
Chanjo ni ya majaribio, na sijaona sehemu mtu akikanusha hii hoja ya Gwajima, zingine ni kelele tu za madalali, tutengeneza yetu kwani ulisikia tunashida ya chanjo ya Corona?
Kwani Gwajima ni nani hadi ajibiwe na WHO? waziri ameshasema clinical trials na tafiti zilionyesha faida ni kubwa kuliko hasara za kutumia chanjo iliyotengenezwa on short notice sasa mpaka hapo unataka majibu gani zaidi ya hayo?

Gwajima hana anachojua kuhusu sayansi.... Si ndio aliropoka kwamba 5G inaleta Covid 19? sasa Leo hii mnamuamini kuwa ni mchambuzi wa epidemiology?

Duh hii nchi ngumu sana
 
Nilimsikia kidogo tu kupitia radio ya E Fm, mie nimemkubali. Hao wanaojiita wataalam ni wa kukopi na kubandika tu. Wasomi wetu wameshindwa kuyarejesha majina ya sehemu zetu ya asili kama mikoa na kadhalika lakini bado tunawaita wataalamu. Aibu.
 
unaweza niambia haya maneno umetoa wapi? Niletee document iliyoandika hiki hapa maana najua ww sio medicine expert.

Wakati bado nasubiri supporting document..... Chanjo zilifanyiwa clinical trials toka mwaka jana na ilirushwa live kwenye Tv. Na mwishoni ndio zikapitishwa kutumika kwa watu wote na sio kweli kwamba zilitoka maabara basi zikaanza sambazwa. Ni UONGO

Kingine Astra Zeneca imezuiwa kwa baadhi ya umri na nchi sababu ya risk tu ila sio kwamba ina makosa. Kuganda damu ni chini ya 0.00001 ya watumiaji zaidi ya million 50 wa chanjo hiyo sasa unaposema ina madhara je umepima ratio??? Hata Kansa katika kila watumiaji 100 fahamu wa tiba ya mionzi duniani 38 kati yao.... YES ni 38!! huwa wanapata madhara ya tiba hiyo tena ndani ya saa 24 za kwanza!! Kuanzia nywele kunyonyoka mpaka viungo kulemaa. Ila sijawahi sikia mkipiga marufuku ocean road!!

Then emergency maana yake ni kasi ya kuprocess na kutoa ruhusa ya chanjo kutumika lakini haimaanishi eti inakua ina mapungufu per se. Kuhusu madhara kisayansi unaweza estimate kwa kutumia data za wakati huo kubashiri huko mbele. Hyo ni kazi ya big data analytics!! Ambayo najua hujawahi isikia.

So mambo ya taaluma waachie WHO ww kabishane simba na yangu tu
 

Hahaahaaa haa haa 😂😂😂😂😂😂!

"So mambo ya taaluma waachie WHO ww kabishane simba na yangu tu."

Timamu, 100% kabisa.
 
Ni wapi sasa wamepingana na gwajima kwamba chanjo si ya majaribio?
 
Sio WHO, hao wataalam wanaodaiwa kumkosoa Gwajima, ni wapi wamekosoa juu ya chanjo kuwa ya majaribio?
 
Nimetoa wapi? Kwahiyo huwa usikilizi hata taarifa za habari? BBC, CNN , Aljazeera nk?
 
Sio WHO, hao wataalam wanaodaiwa kumkosoa Gwajima, ni wapi wamekosoa juu ya chanjo kuwa ya majaribio?
Sasa si ukanunue hilo gazeti usome!! Kwanini unalazimisha majibu yatoke kwa hao wataalamu pekee ilihali naibu waziri ameshajibu? Au unakubali kwamba waziri kapotosha umma.... Yaani daktari kapotosha ila mchungaji aliyebobea kwenye theology ndio yupo sahihi?

Duh
 
Nimetoa wapi? Kwahiyo huwa usikilizi hata taarifa za habari? BBC, CNN , Aljazeera nk?
Umewahi kuandika tafiti kweli? Lazima kila neno la kitakwimu uwe na chanzo cha taarifa kuepuka upotoshaji. Huwezi toa allegations nzito kama hizo alafu unatoa majibu mepesi eti BBC na Al Jazeera?? Embu nitumie link nikasikilize hiyo habari.
 
Kwani heading ya uzi inasemaje?, hebu isome tena. Huyo waziri ndio kasema chanjo sio ya majaribio?
 
Umewahi kuandika tafiti kweli? Lazima kila neno la kitakwimu uwe na chanzo cha taarifa kuepuka upotoshaji. Huwezi toa allegations nzito kama hizo alafu unatoa majibu mepesi eti BBC na Al Jazeera?? Embu nitumie link nikasikilize hiyo habari.
Kwani vyombo vya habari sio source ya taarifa? , Taarifa hizi zipo, fanya search kidogo google, acha uvivu.
 
tukiachana na uzinzi wake,wewe unaweza kumshinda gwajima kwa uelewa wa mambo,
au kujenga hoja??
Unashindanisha zero brain na intellectual? Yaani kuongea povu likitoka kwenye mic ndo hoja? Watu wa lumumba aliyewatoga kweli hakupiga mswaki siku hiyo.
 
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita ,tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje.!!!
Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashqngilia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…