Watabanana hapo hapo

Watabanana hapo hapo

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Ni beti ya wimbo wa pwani!
Bure usijisumbuwe cheo chetu kimoja
Ya nini matusi, ugomvi na mabishano
Kama wewe ni mkewe na mimi keshaniowa
Yanini hasama choyo na kununiana
Kama wewe wa nyumba kubwa mimi ni wa nyumba ndogo
Tutabanana hapa hapa kwa mwanamme mmoja sote tule kwa pamoja!
 
Jamii ya kushabikia nyumba ndogo unategemea nini...kama nawaona akina dada, yaani rusha roho balaa huwa zinaishia na ngumi za kufa mtu.
 
Jamii ya kushabikia nyumba ndogo unategemea nini...kama nawaona akina dada, yaani rusha roho balaa huwa zinaishia na ngumi za kufa mtu.

Mume Hubajeti sawa, wivu na choyo cha nini?
Hakuna cha peke yako hasa hapa mjini
Kugawana na mwenzako siku hizi ni fesheni
Tutabanana hapa hapa hunipiku asilani!
 
Mshindwe na mlegee nyie wa nyumba ndogo! Pepo linawasumbua tafuteni muwe nyumba kubwa
 
Mume Hubajeti sawa, wivu na choyo cha nini?
Hakuna cha peke yako hasa hapa mjini
Kugawana na mwenzako siku hizi ni fesheni
Tutabanana hapa hapa hunipiku asilani!

Sitaki kubanana sitaki kushare, mimi mchoyo. Naona umekuwa mzee yusuph nawewe
 
umenikumbusha kisa kimoja....
kuna binti aliolewa na mume wa mtu.....
akawa anajigamba na kumtusi bi mkubwa kila mara...huu wimbo alikuwa anaupenda sana.......

na hivi walikuwa wanakaa jirani, mwanamke wa watu alikoma, alikuwa anapigwa vijembe daily....

mwisho wa siku bi mdogo akafumaniwa red handed...... kalimwa talaka yake watoto wake wawili wanaishi na bi mkubwa...

sasa hivi ana heshima na adabu,
 
Huyo mume akianza kuharisha nani atamvisha nepi? Au ndio mtabanana kwa hilo pia?
 
Huyo mume akianza kuharisha nani atamvisha nepi? Au ndio mtabanana kwa hilo pia?

Kwani huyu mume ana xxxxxxx mbili? si lazima huo uharo atauharia nyumba moja wakati wa mzunguko wa zamu?
 
Back
Top Bottom