Watafiti wameunda Cement yenye uwezo wa kupitisha umeme Majumbani

Watafiti wameunda Cement yenye uwezo wa kupitisha umeme Majumbani

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833
Cement Electricity _20250421_185346_0000.png



Timu ya Watafiti kutoka chuo kikuu Cha kusini - mashariki nchini China, ikiongozwa na Mtaalam Profesa Zhou Yang, imeunda muundo mpya wa seruji hydrogel (cement) ambayo Ina uwezo wa kuzalisha na kuhifadhi Umeme kwa wakati mmoja.

Teknolojia hii inaweza kubadilisha maisha ya Wanadamu kwa kuweza kusaidia kujenga Barabara au majengo yanayojiendesha Yenyewe. Muundo wake umeundwa kwa kutumia shina ambazo zina hydrogel cement zenye chembechembe za ioni (chuma) ambayo inakupa uwezo wa kubadilisha Joto kuwa umeme.

Kwaiyo watu watakua na uwezo wa kutumia cement kusambaza umeme Majumbani na kuwasha vitu mbalimbali kupitia Mwanga wa jua. Mafanikio haya yataonyeshwa kupitia Tukio la SynBioBeta 2025 ambalo linatarajiwa kupunguza utoaji wa hewa chafu na kufanya ujenzi kuwa rafiki zaidi wa mazingira.
 
Yaan sijaelewa kitu chochote naona mauzauza tu maelezo hayajanyooka fix fix nyingi sana, huo umeme unafanyafanyaje? Mchina unamjua vizuri lakini na iPhone zake za uongo iPhone inauzwa million ya mchina anakuuzia ile ile muonekano ule ule kwa 150,000 tu akili kichwani mwako
 
Back
Top Bottom