Wataka Kufanya Biashara Yako Kwa Kutumia Mtandao?

Wataka Kufanya Biashara Yako Kwa Kutumia Mtandao?

Promota

Member
Joined
Sep 19, 2014
Posts
17
Reaction score
8
Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia ili kuboresha au kufanya biashara yako kwa kutumia mtandao. Katika nchi kama Marekani, Canada, Uingereza na Australia, njia hizi zinatumiwa na wafanyabiashara karibu wote kuanzia makampuni makubwa kabisa hadi zile biashara ndogo za mitaani. Kuna faida nyingi zinazotokana na matumizi hayo ya mtandao katika kufanya biashara. Nitajaribu kuelezea njia chache hapa. Awali ya yote inabidi niombe msamaha endapo tafsiri ya maneno mengine haitakuwa sahihi (tafsiri hizi ni za kwangu mwenyewe), nitaomba tusaidiane pale utakapokuwa na tafsiri sahihi.


Nitatazama njia nne yaani kutumia tovuti (using a website to market your business), Tovuti za simu (mobile websites), mitandao ya kijamii (social media marketing) na Google business listings.




1. Biashara Kwa Kutumia Tovuti


Watu wengi sasa wanatumia kompyuta au simu za mikononi kupata taarifa za kitafiti, kutatua matatizo yao au kununua bidhaa mtandaoni. Kujenga tovuti nzuri na kuitangaza vyema mtandaoni kutasiaidia biashara yako kupata wateja wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi. Faida za kutumia tovuti katika biashara yako ni nyingi mno, hapa ni chache ninazoweza kuzitaja:


- Biashara yako ndogo inaweza ikashindana na kampuni kubwa kabisa, kinachotakiwa ni ubora wa tovuti yako.
- Ni njia ya kuitangaza biashara yako kwa bei ndogo kabisa. Gharama kubwa ni ujenzi wa tovuti yako ambayo nayo itategemea aina ya tovuti, ukubwa wake na kampuni itakayokujengea. Baada ya hapo ni pesa kidogo sana ya kulipia domaina name yako ( kitu kama Tshs 20,000 kwa mwaka kwa kuanzia) na hosting (kitu kama Tshs 120,000 kwa mwaka kwa kuanzia).
- Biashara yako itatangazwa saa 24 kwa siku, siku 365 kwa mwaka. Ukishaweka tovuti yako hewani, wewe unatulia na matangazo yanaendelea muda wote dunia nzima, usiku na mchana. Watanzania na nchi za Afrika tukiwa tumelala India, Japan, Malaysia, China, Marekani wanasoma matangazo yako.
- Ni rahisi sana ku-update taarifa zako, huhitaji kwenda kwenye magazeti au kituo cha TV, ni wewe na na kompyuta yako tena muda mfupi sana. Hii inasaidia kama kuna special promotions, bidhaa mpya nk.
_ Tovuti inapunguza muda mwingi ambao ungeutumia kujibu maswali kwenye simu, kwenda kwenye vyombo vya habari, kuandika barua pepe hivyo kupata muda mwingi zaidi kwa shughuli nyingine za kiuzalishaji.
- Na faida nyinginezo nyingi..


Kama unataka kujua zaidi, soma ukurasa huu (kwa lugha ya kiingereza) kwenye moja ya tovuti zangu hapa: Local Business Marketing In Tanzania - Why You Need A Website For Your Business In Tanzania




2. Tovuti Za Simu (Mobile Websites)


Hizi ni tovuti zinazoweza kuangaliwa vizuri na watumiaji wa simu za kwenye viganja (smart phones, tablets nk.). Njia hii ni njia inayokua kwa kasi sana kwenye nchi zilizoendea kwa sababu ya uwingi wa wamiliki wa simu za mkononi na urahisi wa matumizi wa simu hizo. Mtu atapata taarifa anayotaka akiwa popote pale, akiwa anapata kinywaji, akiwa ndani ya chombo cah usafiri, amepumzika kitandani nk. Hizi ndizo sababu kubwa za umaarufu wa njia hii ya kukuza biashara.


Waweza kuboresha tovuti uliyo nayo ionekane vizuri kwenye simu za mkononi (customization) au ukajenga tovuti mahsusi kwa simu za mkononi kupitia makampuni mahsusi kwa tovuti hizi. Waweza pia kumiliki tovuti hii tuu bila tovuti kubwa zilizozoeleka na ukatanagaza biashara yako vizuri tu. Tovuti hizi zina kurasa chache sana zinazotoa taarifa muhimu tu kama sehemu iliyopo biashara, muda wa kazi, sample za bidhaa (ambazo utabadilisha kila unapopata mali mpya), kufanya booking kwenye hoteli au chombo cha usafiri. Simu hizi ni bora kwa biashara za ndani (local businesses) na zinafaa zaidi kwa biashara kama hoteli, makampuni ya usafiri, taxi, wanasheria, madaktari na mafundi na wengine.


Utatakiwa kutoa gharama ya ujenzi wa tovuti (ambayo ni ndogo) na kulipia hosting kwa mwezi (pesa ndogo kwa mfanya biashara). Mfano wa tovuti hizi ni huu hapa ambapo hii ni tovuti ya Mama Sheila ambaye biashara yake ni ya kuuza viatu vipya hasa vya vijana pale Kariakoo, mtaa wa Narung'ombe. Tazama tovuti hiyo hapa : Home.


Nafikiri ni busara kuishia hapa kwa leo kabla ya kutazama njia nyingine mbili zilizosalia siku nyingine.


Laurian.
 
Back
Top Bottom