Wataka Kutibiwa INDIA Usaidiwe?

Wataka Kutibiwa INDIA Usaidiwe?

Apollo Hospitals

New Member
Joined
Jul 5, 2014
Posts
1
Reaction score
7
Habari wandugu?
Mimi ni mtanzania. Daktari bingwa, niliyefanya super specialization katika magonjwa ya Moyo. Nimebahatika kusoma na kuishi India. Nitakuwa tayari kumpa mwongozo mtanzania yeyote ambaye ana uwezo wa kuja India kupata tiba PASIPO KUMTOZA MALIPO YOYOTE YALE. Mtu atatakiwa anitumie vipimo toka kwa daktari wake kama anavyo, au anitumie maelezo ya ugonjwa wake kwa simu yangu. KWA SABABU YA UFINYU WA MUDA NAWEZA KUCHELEWA KUTOA MAJIBU HADI SIKU TATU. Pia mtu anaweza wasiliana nami moja kwa moja kwa namba +91 90 666 46317 (Email: matibabu.india@gmail.com)

KWANINI NATAKA KUSAIDIA?

Nimeamua kutoa mwongozo huu, maana nimehusika katika kuwasaidia watanzania na wakenya kadhaa ambao walitaka au walishatapeliwa. Mara ya mwisho nimemsaidia mtanzania dada mmoja kutoka Plan International, ambaye alikuwa anang’ang’aniwa kubaki kwenye hospitali fulani kubwa jijini Bangarole; huku uongozi wa hospitali ukijua hauwezi uka offer tiba zaidi.

KUNA MALIPO YOYOTE NITAHITAJI?

SITAHITAJI HATA SENTI MOJA. Nitatoa mwongozo pale nikipata nafasi.

NINA UHUSIANO NA HOSPITALI ZIPI?

Sina uhusiano na hospitali yoyote nchini India. HIVYO siwakilishi hospitali yoyote hapa India. Mimi kazi yangu ni kushauri wapi waweza kwenda kulingana na sifa za hospitali na madaktari. Lakini baadhi wanaweza wakanufaika na contacts za baadhi ya International Patient Managers au baadhi ya madaktari wakubwa katika hizi hospitali.

Kwanini Nimechagua ID ya Apollo Hospitals?

Nimependa kutumia ID ya Apollo Hospitals, maana hizi ni chain za hospitali ambazo zinatoa huduma za kimataifa. Binafsi ninazifahamu zaidi hospitali za Apollo kuliko hospitali nyingine. Pia hii hospitali imeingia mkataba na serikali ya Tanzania katika kutoa tiba kwa watanzania waendao India. Ni hospitali ya kimataifa, inayotambuliwa na kukaguliwa mara kwa mara na Joint Commission International (JCI) ya US, ambayo husimamia ubora na usalama wa tiba zitolewazo na hospitali kwa wagonjwa. Pia ninafahamiana na baadhi ya madaktari bingwa wa vitengo vya Moyo wa Apollo Hospitals. LAKINI SIIWAKILISHI HOSPITALI YA APOLLO. HAPA NATOA MSAADA TU.

KUNA MAFAO YOYOTE NINAYOPATA?

Madaktari wengi Tanzania hupewa percent wakituma wagonjwa India. Bahati mbaya sana, usipomtumia daktari gharama zinakuwa juu zaidi. Mimi sijawahi omba percent yeyote ile kwa wale niliowasaidia katika hospitali husika. Sitegemei kupata percent toka kwa hospitali husika au mgonjwa. NITASAIDIA PALE NITAKOPATA NAFASI.

KUNA HOSPITALI NYINGINE WAZIFAHAMU?

Ninazifahamu hospitali nyingine kubwa kama FORTIS na NARAYANA HEALTH, ambazo pia zina sifa; lakini sina contacts nyingi kama toka Apollo Hospitals.

JE, WAGONJWA WOTE NITAWASHAURI WAENDE APOLLO HOSPITALS?

Ninawajua vizuri wagonjwa wapi wanastahili kwenda Apollo Hospitals, maana Apollo Hospitals nao wamebobea katika baadhi ya maeneo, huku baadhi ya sehemu wakifanya vibaya.

WAGONJWA GANI NITAWASAIDIA?

Nitasaidia wale wagonjwa binafsi, wasiolipiwa na serikali. Wagonjwa wa serikali husaidiwa na muambata wa tiba, aliyeko ubalozi wa Tanzania jijini New Delhi. Bado naweza wapa USHAURI.

KWANINI WATU WANAPENDA KUTIBIWA INDIA?

India ni nchi inayosifika kwa kutoa huduma za afya za kiwango kikubwa na kwa bei nafuu duniani. Kuna kaka mfanyabiashara wa nguo Kariakoo aliyekuja hivi karibuni India kwa matibabu aliniambia chumba alicholala Apollo Hospital ya Bangarole ambacho ni executive, gharama zake kwa siku ilikuwa ndogo zaidi kuliko gharama za siku za hospitali ya Aga Khan jijini Dar - mimi sifahamu.

KWA MAGONJWA YAPI WAWEZA PATA HUDUMA BORA NCHINI INDIA?

Mamilioni ya watu toka mataifa mbalimbali, Tanzania ikiwamo, hutembelea India kila mwaka kwa ajili ya kufanya medical check na pia kupata tiba kwa magonjwa mbalimbali ambayo yamekosa wataalamu wa kutosha nchini kwao. India ina hospitali kubwa zinazotoa huduma za kiwango cha kimataifa katika kiwango cha ubingwa na ubingwa wa mabingwa katika maeneo mengi machache yakiwa yameorodheshwa hapo chini:
1.Heart Surgery (Upasuaji wa Moyo)
a. Upasuaji wa moyo (Cardiac Surgery)
b. Kuotesha mishipa ya damu ya moyo (Coronary Bypass)
c. Kucheki moyo (Heart Check)
d. Kubarishwa valve za moyo (Heart Valve Replacement)
2.Kuoteshwa Viungo (Organ Transplant Surgeries)
a. Kuoteshwa Ini (Liver Transplant)
b. Kuoteshwa Figo (Kidney Transplant)
c. Kuoteshwa urojorojo wa mifupa (Bone Marrow Transplant)
3.Operesheni za mifupa (Orthopedic Surgery)
a. Kubaridisha vifundo (Total Knee Replacement )
b. Kubadirisha nyonga (Hip Replacement)
c. Kubaririsha viungo (Joint Replacement)
4. Kuweka vifaa vya kusaidia kusikia kama Cochlear Implant hususani kwa watoto walioacha kusikia kutokana na matatizo yaliyotokea utotoni.
5.Tiba za Macho (Eye Care & Treatment)
a. Lasik - Laser Surgery
b. Upasuaji wa Cataract (Cataract Surgery)
c. Upasuaji wa glaucoma (Glaucoma Surgery)
d. Upasuaji wa retina (Retinal Surgery)
6.Upasuaji wa urembo (Cosmetic Surgery)
a. Kukuza matiti (Breast Enlargement)
b. Kunyanyua uso (Face Lift)
c. Upasuaji wa pua (Nose Surgery)
d. Kuotesha nywele kwenye vipara (Hair Transplant)
7.Tiba za Meno (Dental Care)
a. Kutengeneza tabasamu (Smile Design)
b. Meno (Dentures)
c. Upasuaji wa kinywa (Oral Surgery)
8. Tiba za kisasa za saratani (Advanced Cancer Therapy)

JE, NAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA LIPI?

Kuanzia upatikanaji wa viza jijini Dar es Salaam, Barua ya rufaa ya kuletwa India, Hospitali ambayo itamfaa mgonjwa kushughulikia tatizo lake, Kukupa trick za kuhakikisha mgonjwa hazidishiwi gharama, Kuepuka kulazwa wodini kwa muda usiostahili ili kuongeza gharama, Kupata tiba stahili na kwa bei stahili na kupata malazi kwa bei za kurusha.

JE, WASEMAJE KUHUSU TIBA NCHINI INDIA?

Tiba nchini INDIA ipo juu sana. Huwezi ukailinganisha na nchi kama Afrika Kusini, Egypt, na baadhi ya mataifa mengi tu ya Ulaya na Asia, maana ipo juu sana. Wana karibu kila daktari na kifaa kilichopo Duniani kwa ajili ya tiba. SHIDA MHINDI NI MHINDI TU. Anaweza akaandika kwenye file na kukupa dawa kesho wakadai ulipie consultation fee japo hukuonwa na daktari!!! Ukienda Hospitali Fulani, Usanii ni zaidi ya Bongo!!! Unatibiwa wima wima. Mbaya zaidi madaktari wengi wahindi huwa hawasemi ukweli. Wanaweza kukupa false hope kwa kitu ambacho wanajua hawatofanya lolote kuokoa uhai. Magonjwa kama cancer iliyo katika hatua za mwisho wanaweza wakalazimisha kufanya hata procedures ambazo kitabibu ni unethical. Hata kama una pesa, usiingie INDIA kichwakichwa.

JE, NINA ACCOUNT NYINGINE HAPA JAMIIFORUMS?

Ndiyo, nina account nyingine hapa Jamiiforums. Nimeamua kufungua account hii makusudi kwa ajili ya watanzania ambao wana nia ya kutaka kupata matibabu ya kiwango cha juu nchini India. Bahati mbaya kwa kukosa uelewa wamekuwa wanateseka.

KUMBUKA: Mhindi ni Mhindi tu.

Kwa mawasiliano zaidi:
Email: matibabu.india@gmail.com
Tel: +91 90 666 46 317
 
Safi sana. Unafanya jambo jema.

Ushauri wangu, kutokana na umuhimu wa huduma unayotoa ni vema ukawa na verified ID.
 
KuNa mzee wangu nipo nae hapa kalalamika sana alikuwepo india wamemfanyia usanii, jombi shukran tutakutafuta
 
Vipi kuhusu wale low income clients mkuu, kuna namna ya kuwasaidia kama mkopo katika matibabu then baadae waandaliwe utaratibu wa kurejesha hela hizo mahali husika?
 
kwa taarifa uliyotoa kiukweli ebu tuwie radhi yaani hamna fedha hata senti ya kuchangia ,bas tutashukuru sie
 
forts hospital ni nzuri ila ina watu wa kati (madalali) wengi. bill halis hupanda hata kwa zaidi ya asilimia 50. nadhan utakuwa msaada mzuri hata kama utaintroduce fee kidogo si mbaya muhimu uwe na msaada mzur
 
Wewe utakuwa ni agent wa Apollo Hospital. Mimi nimetibiwa Max Super Speciality Hospital, ipo New Delhi ambako nilifanyiwa Spine Surgery na Dr. Bipin Walia. Nilienda kichwa kichwa tu baada ya kupata email ya Assistant Manager for International Patients na kuwasiliana naye. Diagnosis waliyofanya ilokuwa ni sawa na iliyofanywa na Prof. Kahamba wa Muhimbili Orthopedic Institute. Nilifika na kufanyiwa bipimo siku hiyohiyo na kesho yake nilifanyiwa operation. Baada ya siku 3 niliruhusiwa na nikatafutiwa Hotel (huko zinaitwa BB) nilikokaa hadi nilipotolewa nyuzi. Nilifurahia huduma zao na hakuna utapeli hata kidogo

Lakini pia, hivi karibuni, dada yangu mwenye tatizo la Moyo ametibiwa The Madras Mission Hospital, Chennai na kufungiwa piece marker. Tulimpeleka kule kama familia.

Mwisho, naomba niwaeleze kwamba Medical Attache aliyeko Ubalozi wa TZ huko India (New Dehli) amekuwa pia alitoa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaokwenda kutibiwa India bila kujali kama wanakwenda kwa gharama za Serikali au za binafsi. Mtu yeyote akiwasiliana naye na kumtumia vipimo kutoka Local Doctors anaweza kumsaidia kutafuta Hospitali za bei nafuu sana kulingana na tatizo la mhisika

Medical Attache wa Tanzania Dehli ni Dr. Kheri O. Goloka, na nambari yake ya simu ni +919958471668
 
Back
Top Bottom