#COVID19 Watakaochanja chanjo ya Corona kesho kuingia bure uwanja wa taifa, hii sio siasa?

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Wizara ya Afya kesho watatoa tiketi za bure za mechi ya Simba na Yanga kwa wale watakaokubali kuchanja siku ya kesho.

Kwanza kabisa naipongeza Wizara ya Afya kwa ubunifu huu, ila kuna jambo litaonekana haliko sawa.
Chanjo ya corona ikiendelea kuwekewa zawadi hizi ni kutengeneza zaidi mashaka badala ya kupunguza mashaka.
Wapo wataojiuliza kwa nini iwe hivi?
Wizara ilipaswa iendelee kutoa elimu juu ya watu kupata chanjo. Ila kuweka hizi zawadi kunazidisha maswali.

Wizara haioni kwamba wale waliochanja na ni wapenzi wa soka, hawana uwezo wa kununua tiketi watakuwa wanajilaumu sana?

Yote kwa yote kila la kheri!
 
Ofa hii ni kwa mbumbumbu fc tu wananchi hatuhusiki hayo maana sisi ni wapenzi wa soka hata Bila ya ofa kama hizi (rejea takwimu za t.f.f)
 
Uchanje uingie Bure uwanjani kwani ikichanjwa hakuna mabadiliko ya mwili? Usijekuwa unaingia uwanjani kusinzia mwanzo mwisho!!!!
 
Watahangaika sana lakini wajue kitu kimoja Mungu wa Mbinguni hadhihakiwi na hulipiza kisasi hadi kizazi cha nne.
 
Uchanje uingie Bure uwanjani kwani ikichanjwa hakuna mabadiliko ya mwili? Usijekuwa unaingia uwanjani kusinzia mwanzo mwisho!!!!
Labda waseme chanjo itakupa nguvu za ziada kupigana vikumbo kuingia uwanjani. Hapo wanaweza pata 'wateja'.
 
Chanjo mbona n nzur tu nguvu Kubwa Sana ya nn ndomana watu wanakuwa waoga kuchanja
 
Mi ntachanja siku hoja za Gwajima zitakapo jibiwa kwa ufasaha[emoji2223][emoji2223][emoji2223]
 
Hata kama wakisema ukichanja unapewa Milioni na papuchi juu SICHANJI
 
Wanatengeneza mazingira ya chanjo hii kuogopwa na jamii. Why promo
 
Ni Tanzania tu kila jambo ni kumfurahisha mwanasiasa. Haingii akilini chanjo inasababisha matatizo kwa wengine mpaka kufa then TFF inasisitiza watu waende kuchanjwa kitu ambacho ni hatari.
Kuna Mtanzania yeyote aliyekufa kwa sababu ya Chanjo?
 
Uchanje uingie Bure uwanjani kwani ikichanjwa hakuna mabadiliko ya mwili? Usijekuwa unaingia uwanjani kusinzia mwanzo mwisho!!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…